MAZOEZI HAYA YATAWEZESHA KUMTOA KNOCK OUT MWANAJESHI… Inategemea tu unahitaji kupata nini.

Mwili wa binadamu unahitaji mazoezi pengine kwa kiasi kikubwa sana kwa sababu nyingi ikiwemo, kuongeza brain receptors, ku-manage insulin mwilini na kuzuia magonjwa.

Ufanyaji wa mazoezi unatofautiana na kiwango cha mtu na mtu, wapo wanaofanya mazoezi kwa ajili ya afya tu, na wengine wanafanya mazoezi kama sehemu ya kazi zao.

Kuna tofauti kubwa ya ufanyaji wa mazoezi kati ya mwanajeshi (marine) na kijana anayetafuta six pack tu za kuonesha Instagram, na mwanriadha.

Mwanajeshi anafanya mazoezi kwa ajili ya kujitengeneza awe na uwezo wa kumuua adui kwa urahisi, na awe mgumu sana kuuliwa na adui. Hivyo mazoezi ya mwanajeshi ni ya kufa na kupona.

Mwanariadha anafanya mazoezi ili ashinde mataji, mazoezi yake huwa ni tofauti na mara nyingi huwa yana focus maalumu ya kumuongezea ufanisi kwenye eneo la kukimbia.

Hii ni aina ya mazoezi ambayo inafanywa na mwanajeshi ambaye amekuwa mwanajeshi FIT zaidi katika mashindano yanayofanyika kila mwaka baina ya wanajeshi. Ultimate Tactical Athlete competition.

Sgt. Ethan Mawhinney baada ya kushindwa kuwa wa kwanza kwenye mashindano hayo mwaka 2015, alirudi kujinoa zaidi na kwa ufupi hii routije ndio imempandisha.

Explosive routines

Hii ina maanisha, kila zoezi unalofanya linafanyika kwa kasi na ngvu za hali ya juu. Kama ni kukimbia, program inakuwa ni kukimbia kwa kasi kwa mbio fupi fupi au short distance sprints.
Hapa kila zoezi unalofanya, linakuwa ni kwa nguvu na kasi ya hali ya juu huku ukijipa muda mfupi sana wa kupumzika kati ya zoezi moja hadi jingine.

Push ups

Hili ni zoezi linafanywa na watu wengi duniani. Push ups zinakujenga kuwa na nguvu, na kufanya kazi kwa muda mrefu bila kuchoka. Unaweza ukaangalia jinsi ya kufanya Push-ups kwa usahihi hapa.

Explosive push ups zinakujenga zaidi kwani unatumia uzito wa mwili wako kujijenga. Faida za push ups ni nyingi zaidi ya kunyanyua uzito gym kwa sababu push ups ikifanyika ipasavyo, inaushuhulisha mwili wako wote.

Box Jump

Hii ni moja kati ya mazoezi yanayohusisha sehemu kubwa ya mwili kuanzia mikono, torso (kiwili wili) pamoja na miguu kwa sana. Tazama hapa jinsi ya kufanya Box jump kwa usahihi.
Olympic weightlifting.

Zoezi hili ni muhimu sana katika kujenga perfomance ya hai ya juu kwenye mwili wako. Ni zoezi ambalo mara nyingi linahitaji kujifunza na kulizoea taratibu kwa sababu linahitaji ufanisi kuzuia kujijeruhi.
Cheki hapa uone jinsi unavyoweza kulifanya zoezi hili kwa ufanisi.

Kama huna haja ya kushiriki katika mashindano au wewe sio mwanajeshi, yapo mazoezi marahisi ambayo yatakusaidia.

 

Kama una lolote la kuongeza kuhusu article hii nicheki kwenye Facebook au Twitter au tudondoshee comment hapa chini.

Writer : Abdulkweli

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com