HIZI NDIO VITA 10 ZILIZO MALIZA WATU WENGI ZAIDI DUNIANI?… Marekani na Korea itakuwaje?

1. WWII


Adolf Hitler na Nazi Germans walipojaribu kuvamia na kuitawala Ulaya 1939, karibu dunia nzima ilipigana vita hii ambayo mpaka sasa katika rekodi ndio vita iliyochukua maisha ya watu wengi zaidi kwa kipindi chote cha mapigano.

Watu milion 66 walikufa katika vita hi. Katika kila saa moja ya vita hii inakadiriwa kuwa walikuwa wanakufa watu 1256. ni moja kati ya vita mbaya sana kuwahi kutokea ulimwenguni.

Vifo: 66,000,000

2. WW I


1914 hii ni vita ya Kwanza ya dunia na ilikuwa ni kati ya Uingereza, Russia, na Ufarasa kwa upande mmoja huku upande wa pili kulikuwa na Italy, Austria, Ujerumani na Hungary.

Vifo: 16,280,000

3. The Holocaust


Mauaji ya Jewish na jamii zingine ndogo. Mauaji haya yalipewa sapoti na serikali ya wa – Nazi. Mauaji haya yalitokea na kufuatiwa na vita kuu ya pili ya dunia.

Vifo: 16,315,000

4. Russia civil war
Baada ya mapinduzi ya Urusi, vilizuka vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1917 na kupoteza maisha ya watu wengi.

Vifo: 9,000,000

5. Chinese Civil war


Mwaka 1945 haukuwa mwaka mzuri kwa China maana vita hii ilianza muda mfupi baada ya vita ya pili ya dunia kumalizika. Na ilikuwa ni vita kati ya chama cha wakomunisti na serikali ya China ambao waliungana na kupambana na uvamizi wa Japan.

Vifo: 5,000,000

6. Flight and expulsion of German
Hii ilikuwa baada tu ya vita kuu ya dunia kumalizika. Hizi zilikuwa violence wakati wa raia wa Ujerumani ambao walilazimika kuhama katika maeneo ambayo Ujerumani ilikuwa inayashikilia, hasa maeneo ya Poland.
Vifo: 2,100,000

7. Sudanese civil war
Vita ya kwanza ya wenyewe kwa wenyewe ya Sudan mwaka 1983 ilichukua maisha ya wengi. Vita, njaa, na magonjwa viliwamaliza watu 2,000,000.

8. Eritrea War of Independence
Vita ya nchi ya Eritrea na Ethiopia ilikuwa miaka ya 1962, ilichukua maisha ya watu zaidi ya milioni 2, na kikubwa kilichoua watu wengi ukiachilia mbali mapambano yenyewe, ilikuwa ni njaa na magonjwa.

9. Red Terror Ethiopia
Mwaka 1975 ilikuwa ni shida nchini Ethiopia maana kulikuwa na mauaji ya kutisha ya wale wote wanaopinga uongozi wa Colonel Mengistu.

Vifo: 1,500,000.

10. Vita ya Korea
Hii ni vita ile ya kipekee kwa sababu ilihusisha Korea kusini ambayo ilikuwa inapewa sapoti na Marekani dhidi ya Korea Kaskazini ambayo ilikuwa inapewa sapoti na China. Mtiti huu ulichukua maisha ya watu 1,170,000.

Zipo vita nyingine zilizochukua raia wengi sana na hizi 10 ndio zimenigusa zaidi kwa idadi ya waathirika. Je ni vita gani unayoijua iliyomaliza watu wengi sana? Najua kunaMajimaji iliyoua 175,000, Rwanda genocide watu 800,000, Niregia War watu milioni 1 na nyinginezo, but nitafurahi ukinipa na wewe list yako.

 

By: Abdulkweli watupipo

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com