HIVI NDIO VYAKULA 6 VYA BEI RAHISI ZAIDI DAR ES SALAAM, HUWEZI KUFA NJAA USWAHILINI.

Kuna usemi unaosema mwili haujengwi kwa tofali na mwingine wa mtaani ukisema “kambi popote” yaani riziki hupatikana mahali popote na kwa kufanya shughuli yoyote ile.

Katika jiji la Dar es salaam yapo maeneo mengi ambayo yanasifika kwa biashara mbalimbali, maeneo ya uswailini maarufu kama uswazi biashara mbalimbali hufanyika na watupipo.com imekusogezea biashara 6 maarufu maeneo hayo.

Biashara ya miguu ya kuku.

Biashara hii mara nyingi hufanyika wakati wa usiku ambapo wanafunzi wengi huonekana wakinunua miguu ya kuku, supu ya utumbo wa kuku, vichwa vya kuku yaani hapa kuku huliwa kila kitu hehee. Mama Arapha ni moja ya wafanyabiashara wa miguu ya kuku anasema wateja wengi ni wanafunzi na kina mama hasa nyakati za usiku.

Biashara ya Pweza

Kwa wale wapenzi wa samaki bila shaka wanamekutana sana katika meza zao za vyakula vya mtaani. Samaki huyu afahamikaye kama Pweza. Majira ya usiku katika maeneo ya uswailini utakutana na biashara hii kwa wingi ambapo wateja wengi wanakua ni wanaume.

Biashara ya nyama ya kuku.

Hii hapa ni tofauti na ile ya miguu ya kuku, yaani hapa unaweza kupata kipapatio, upaja pamoja na kidari cha kuku kwa bei ya kawaida kabisa. Wateja wengi huenda kuunga kama mboga na pengine kama umewahi tembelea ndugu yako  uswailini siku moja labda umewahi kula vyuku wa aina hii.

Biashara ya samaki.

Giza likiwa linaanza kuingia tu, utawaona hasa kina mama wakiwa na vikapu pamoja na meza kwa ajili ya kufanya biashara hiyo. Hapa huuza samaki wadogo wadogo na unaweza kupata fungu moja kwa shilingi elfu moja tu na kwenda kula ugali safi kabisa.

Biashara ya vitumbua.

Utashangaa sana pale ambapo utaona vitafunwa vinauzwa majira ya usiku, lakini wala haina haja ya kushtuka maana uswailini ni kawaida sana kukutana na biashara hii. Mara nyingi utakutana na kinabibi au mara nyingine watoto wakiuza vitumbua hivi.

Biashara ya kahawa

Tofauti na wale wanaotembeza kahawa kwa wanywaji maeneo mbalimbali wapo ambao wana vijiwe vya kuuzia kahawa, hapa utawakuta watu mbalimbali wazee na vijana wakinywa kahawa huku wakisindikiza na story hasa za michezo.

Sina shaka ume enjoy na umefahamu juu ya biashara za maeneo ya uswailini ama uswazi jijini Dar es salaam, kazi kwako kuja kujionea na pengine kuwa mdau wa moja kati ya biashara hizi.

Kama huna ajira… Fikiria namna unavyoweza kuziongezea thamani biashara hizi ili na wewe upate mkate wako.

 

Charles Kombe

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com