Mauaji sio kosa…! Haya ndio maajabu ya kisiwa cha Sentinei

Kuanzia Brazil mpaka Asia na India, zipo habari kuhusu makabila ambayo bado yanaishi kama ilivyokuwa miaka ya stone age. Hizi ni sifa 5 kutoka katika kabila la ajabu Magharibi mwa India katika kisiwa cha Sentinei kilichotajwa na mitandao mingi ikiwemo millardayo.com kuwa kisiwa hatari zaidi.

Kabila wanaloishi watu wa kisiwa hiki wanajulikana kama Sentenese ambao mpaka leo wanaishi maisha yanayojulikana kama hunting and gathering. Kuwinda na uokotezaji au ukusanyaji ili kuishi. Ni kweli kwamba hiki ni kisiwa cha ajabu.

Idadi ya watu

Mpaka sasa hivi inakadiriwa kuwa kuna watu zaidi ya 300 katika kisiwa hiki. Mwaka 2004 wakati wa Tsunami iliyotokea duniani na kuua watu zaidi ya 200,000 iliaminika kwamba kabila hili la Sentinelese lilimalizwa katika mafuriko hayo.

Siku tatu baada ya mafuriko helikopta ya serikali ya India ilipita juu ya Kisiwa hicho ili kuangalia athari pamoja na kudondosha msaada wa chakula, wanaume wa kabila hilo walijitokeza na kuifukuza Helikopta hiyo.

Watu hao walistukia kuja kwa Tsunami wakawahi sehemu ambazo maji hayakuweza kuwafikia.

Jaribio la serikali kuwasogelea watu hao

Serikali ya India miaka ya 70 walifanya majaribio ya kutengeneza urafiki na watu wa kisiwa hicho kwa kupeleka zawadi kama vile ndizi, nazi na vitu vingine lakini watu hao walichukua vitu hivyo na kuwarushia mishale waliovileta.

Sometimes watu hao walijitokeza kuonesha kwamba ni marafiki lakini wakishachukua vitu hivyo waliwafukuza.

Mwaka 1995 serikali iliamua kusitisha majaribio ya kuwafikia watu hao ambao inasemekana wameishi katika kisiwa hicho kwa zaidi ya miaka 60 according to millardayo.com.

Maisha yao

Watu wa kabila la Sentinelese wanaishi katika nyumba zilizojengwa kwa kutumia miti. Kuna nyumba kubwa ambazo zinachukua watu wengi na zipo nyumba ndogo kwa ajili ya familia lakini pia zipo nyumba za muda mfupi ambazo ni kama vibanda vilivyoezekwa bila kuwa na kuta.

Wanaume wanavaa headband na kubeba mishale pamoja ni mikanda minene, huku wanawake wanavaa strings kiunoni na vitu vingine vinabaki wazi wazi. Hawajui maswala ya chupi.

Kwa nini wanaitwa kabila la miaka ya mawe

Hawajui suala la kilimo, hivyo mlo wao mkuu ni nazi, samaki wanaovua kutoka kwenye maji mafupi, na viumbe wengine wa majini kama kobe au ndege wadogo wanaopatikana katika kisiwa hicho.

Mauaji ni kitu cha kawaida

Katika kisiwa hiki mtu yeyote kutoka kwenye ulimwengu wetu ulioendelea anatakiwa kuuawa. Hakuna tafiti zilizofanywa kisiwani humo kwa sababu ni vigumu kufika au kufanya mawasiliano.

Serikali ya India iliamua kuwaacha watu hao waishi kwa amani bila kuingiliwa kwa kuwa wameweza kuishi peke yao kwa miaka yote ya maisha yao.

Hivi karibuni kumekuwa na fununu kwamba serikali ya India na kampuni ya Barefoot resort ina mpango wa kuanzisha safari za kitalii katika kisiwa hicho. kampuni hiyo imekanusha fununu hizi japokuwa inaonekana kunaweza kuwa ni fursa nzuri ya utalii wa thamani zaidi. Kitendo hiki kinaweza kuharibu thamani ya kabila hilo

Unaweza kuongeza chochote kwenye article hii kwa kuacha ujumbe au kutuma email via watupipo.com@gmail.com au tucheki kwenye Facebook na Twitter

Sikiliza radio stations bora za Afrika mashariki kupitia watupipo. Chagua radio juu kabisa kwenye Listen to live radio

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com