ATTENTION EAST AFRICA: Kaa tayari maana mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha. Unajiandaaje?

Niaje, Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania imetupatia tahadhari kuwa mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha, kiasi ambacho hakijawahi kuonekana kwa miaka kadhaa. Mvua hizi zitanyesha katika maeneo yanayozunguka ziwa Victoria.

Maeneo:
Mwanza, Shinyanga, Kagera, Mara, Geita, na Simiyu. Lakini pia maeneo ya Kisumu, Kericho, Kisii na Kakamega hapa Kenya yatarajie mvua hizi kutokana na ukaribu bila kusahau Entebe na Masaka Uganda.

Ushauri: Kwa watupipo wanaishi maeneo hayo, habari hizi zina maana mbili.

Moja: Hii ni neema kwetu na wakulima mjipange kuingia shambani na kutengeneza pesa na chakula kwa nchi zetu za Afrika mashariki.

Mbili: Hizi ni habari za kutisha kwa ndugu zangu mnaishi maeneo ya mabondeni na kwenye mikondo ya maji. Inasemekana mvua hizi ni kubwa kwa hiyo uwezekano wa mafuriko kutokea ni mkubwa pia.

Angalizo:
Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, mvua zimekuwa hazitabiriki sana, hivyo huenda hizi mvua zinaunekana kuwa zitanyesha kuanzia Nov-April lakini zikanyesha kwa muda mfupi zaidi.

Kwa wakulima ni afadhali kuwasiliana na wataalamu wa shamba na kuchagua mazao yanayoweza kulimwa kwa muda mfupi.

Ni hayo tu kutoka Mamlaka ya hali ya hewa ya Tanzania. Ningependa kusikia maoni yako au kama una lolote na kushare na watupipo.com

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com