Roma kakosea kumkataza mtoto wake kuimba ngoma ya Weusi?

Mara kadhaa Roma amewahi kusikika kwenye interview akisema kwamba mbali ya yeye kuwa Rapper, lakini pia ni baba wa familia. Hii ameirudia pia kwenye ngoma ya Zimbabwe ambayo ilikuwa ngoma yake ya kwanza kuvunja rekodi ya kutazamwa zaidi kwenye mtandao wa Youtube.

Jumatatu 23 October, Roma aliweka kwenye mtandao video fupi akiwa na mtoto wake Ivan ndani ya gari, huku ngoma ya madaraka ya kulevya ya Weusi ikipigwa.

Mtoto wa Nyoka ni Nyoka, Ivan alionekana akiimba sambamba na akina Joh Makini kitu ambacho hakikumfurahisha Roma, ambaye alimkataza na kumwambia anatakiwa kuimba nyimbo za shule na sio Bongo fleva.

“Hizo nyimbo hazitakusaidia unatakiwa kuimba nyimbo za shule” Na kwa pamoja wakaanza kuimba nyimbo za shule.

Watanzania walifunguka mitandaoni wengi wakimsifu Roma kwa kumkanya mtoto na kuonesha upande wake wa kuwa kama baba bora… na wengine pia walikuwa na maoni tofauti na kusema hata hizo nyimbo ambazo Roma hataki mtoto wake aimbe, yeye ndio alimuwekea.

Leo katika kipindi cha Leo tena kinachorushwa na Clouds fm radio ya watu, mtangazaji Jose Mara alileta mada hiyo mezani.

Musa Husein: Roma anamkataza mtoto kuimba nyimbo au ni kwa sababu ni nyimbo ya Weusi? Au ana bifu nao.

Dahuu: Wewe acha uchonganishi, wewe sasa ndio utasababisha bifu.

Musa: Lakini Roma yeye ndio mwenye makosa, kwani ukimkataza mtoto kuimba nyimbo ndio atakua daktari?

Dahuu: Mimi naona Roma angetumia njia nyingine kwa kuwa mtoto huwezi kumkataza kwa kukemea.

Mara: Kwani Dahuu wewe angekuwa mtoto wako anaimba ungemuacha.

Dahuu: Ningemkataza lakini nisingemkaripia, maana nilimsikia Chris Mauki akisema hiyo sio njia nzuri ya kumkataza mtoto kitu, ningemuongoza kwa mifano.

Musa: Mi naona Roma amekataza kwa kuwa ni wimbo wa Weusi… Ingekuwa ni Zimbabwe inapigwa hapo angemkataza?

Dahuu: Acha zako Musa hiyo bifu unaisema wewe.

Baadhi ambao tunamfahamu mtangazaji Musa Husein wa Clouds Fm ni mtangazaji mwenye Masihara mengi sana… na mara nyingi amekuwa akitoa comments ambazo zinaweza kukufanya umchape kofi kama uko karibu.

Lakini pamoja na Masihara ambayo Musa alikuwa akiweka kwenye stori hii kuhusu Roma kumkataza mtoto wake asiiimbe Bong oflava, pamoja na comment za watanzania wengine wengi.

Musa aliongea kitu kimoja ambacho hata mimi nimekifiria mara tu nilipoona video ya Roma. Kwanza Roma amefanya kitu kizuri kuweka video ile kwenye mtandao ili kama kuna baadhi ya fans wake ni watoto wakiiona watafikiria mara mbili kabla ya kukariri nyimbo za Bongo fleva na kusahau masomo.

Pili, Roma anatakiwa afanye kazi ya ziada katika kumzuia mtoto wake access ya nyimbo kama hizo na sio kumkataza kwa maneno.

Kwa jinsi Ivan alivyokuwa anafuatisha Madaraka ya Kulevya, inaonekana kwamba ameshaimba hii ngoma mara kadhaa mpaka anafaifahamu. Inaonekana kwamba akiwa nyumbani ngoma zinapigwa na anapata wakati wa kuzisikiliza na kukariri.

Roma anatakiwa atoe maelekezo haya kwa waangalizi wa Ivan ili asipewe access ya kusikiliza ngoma za ambazo haziendani na umri wake na shule.

All in all, nampa big up mwanangu Roma kwa kuonesha mfano mzuri wa kujenga tabia ya mtoto… sisi watu wa nje tutakuwa na maoni yetu ambayo pengine yanaweza kuongeza ufanisi wako, hivyo yale maoni yasioyofaa yaache kama yalivyo na maoni yanayofaa yachukue.

Kama una lolote la kuongeza kwenye article hii please nistue kwenye watupipo Facabook aua Twitter. Zaidi endelea kusikiliza radio online kupitia listen to live radio stations hapo juu.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com