Mwanamke mfanye mwanaume akutumikie utakavyo kwa mbinu hizi

Nimeshakaa na wanawake marafiki na wasio marafiki mara nyingi na kusikiliza mazungumzo mengi kuhusu mahusiano. Kwanza kabisa niseme naheshimu upeo wa akili ya mwanamke, na jinsi anavyopambanua mambo na utofauti uliopo kati mwanaume na mwanamke.

Kwa haraka tutakubaliana kuwa akili (brain) ya mwanamke na mwanamme zimeumbwa na tofauti ndogo ndogo katika utendaji kitu kinachotufanya kuwa na feelings tofauti na namna tofauti ya utendaji wa kazi.

Mfano wa haraka ni kwenye ‘feelings” mwanamke na mwanaume wanatofautiana na jinsi ya ku-deal na feelings zao, na hii ni kutokana na utofauti wa “brain” zao zilivyoundwa katika utendaji.

Miaka ya sasa ni kawaida kusikia mwanamke akiweka wazi vigezo vya mwanaume anavyovitaka, na kati ya mengi ambayo unaweza kuyasikia kwa wanawake tofauti, “upendo, uwezo wa uchumi” ni vitu ambavyo utavisikia kwa wengi.

“Mimi nataka mtu anayejali hisia zangu, mtu anayenipenda kwa dhati na kunipa muda wa kutosha kuwa nae” hili ni moja kati ya jibu nililopata kwa rafiki yangu Mishi, nilipomuuliza sifa za mwanaume anayemtaka.

Lakini tukichukua sifa hizi na kuangalia jinsi ubongo wa mwanaume ulivyoumbwa, system ya kupokea na kutoa feelings haiko sawa na ya mwanamke.

Hata linapokuja suala la kukaa pamoja kwa muda mrefu, mwanaume hajaumbwa kutulia sehemu moja kwa muda mrefu.

Lakini japokuwa tunazo tofauti hizi katika maumbile ya ubongo, bado tunahitaji kujua namna gani tunaweza kukaa pamoja katika mahusiano bila kutokea mifarakano ya mara kwa mara.

Wanawake hushindwa kuelewa wanaume katika baadhi ya mambo haya yafuatayo na hii husababisha shida kwenye nyumba.

1. Mpe nafasi anayotaka

Mwanamke anapenda kupitia kila aina ya feeling katika matendo yanayotokea. Tofauti na mwanaume anayefanya jambo moja na linapokwisha anahama kabisa kwenye jambo lingine na hawezi kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja. Hii ni nature ya ubongo wa mwanaume.

Ukitaka usimkere au usijisikie vibaya kwa kuhisi labda jamaa hana time na wewe, mpe nafasi yake. Ukiona yuko bize na jambo ambalo analijali, usijaribu kumzongazonga kwa maneno au hata kwa vitendo kwa sababu ni rahisi kumhamisha kutoka kwenye concetration yake kabisa, na hili anaweza asilichukulie vizuri.

Mwanaume anahitaji nafasi ya kutosha ili akupe nafasi ya kutosha.

2. Kuwa msaada kwake

Hiki ni kitu ambacho vijana wengi tumeshindwa kukifanya. Na hapa nitazungumzia mtazamo wangu tu kwa jinsi ninavyoelewa na utafiti niliofanya kutka kwa watu wanaonizunguka.

Mwanaume ana uwezo mkubwa wa kufanikisha mambo physically na hata mentally.lakini mwanaume ni kiumbe ambaye hawezi kufanikiwa bila kuwa na msaada pembeni yake.

Wanawake wengi wamejijengea utamaduni wa kutegemea kila kitu kutoka kwa mwanaume na kutegemea mwanaume awe kama Mungu mtu kwao. Hii itakufukuzisha kutoka moyoni mwa kila mwanaume.

Kaa ukijua kuna vitu ambavyo vimeumbwa ndani ya uwezo wako ambavyo mwanaume wako anavihitaji ili afanikiwe kwenye mambo yake na pia kukufanikishia wewe mambo yako. Maisha ya mwanaume na mwanamke yanategemeana.

Ukiijua safari ya maisha anayoielekea mwanaume wako, itazame kwa makini na utafute namna ya kumsaidia. Kuwa makini mwanaume hapaswi kuona kuwa unamzonga katika maamuzi, msaidie yeye afanye maamuzi vile unavyoona yanafaa.

Kifupi jiweke kwenye nafasi ya kuwa msaada kwa manaume uliye naye na usiwe wewe ndio unategemea msaada pekee.

3. Usiombe ombe pesa.

Hii sitasema kwa sana ila nataka tu kuwa clear. Kuna baadhi ya wanawake ambao wamekaa kimatumizi matumizi tu. Kila siku yeye anatengeneza namna ya kutumia pesa iliyoko. Kila siku lazima aombe pesa.

Ukitaka mwanaume akae na kukuona una thamani kwake mfanye kila wakati abaki na pesa. Hapa simaanishi usiombe kabisa pesa pale unapohitaji… Hapana. Namaanisha uhakikishe unacheza na mtu wako katika matumizi sahihi ili asifikie wakati akakuona wewe ndio shimo linalonyonya pesa yake yote.

Jiulize hata kama jamaa ana pesa ya kutosha… kwa nini wewe hutafuti zako hata kama ni kidogo kwa ajili ya kutatua mahitaji madogo madogo uliyonayo?

Kwa nini usioombe akusaidie na wewe kutengeneza pesa zako ukampunguzia mzigo? Kwa nini kila unapopiga simu wazo la kuombwa pesa linakuja akilini mwake?

Je wewe thamani yako ni pesa kama ilivyo kwa bidhaa zingine madukani?

Hapa narudi tena kwenye point  ya hapo juu… Kuwa mshauri mzuri kwenye masuala ya kifedha. Atakuheshimu na kukupenda tu.

4. Mfanye akufukuzie.

Wanaume tumeubwa kwa ajili ya kuwinda. Hata zamani wakati wa stone age, wanaume walikuwa wakiwinda na wanawake walikuwa gatherer.

Baadhi ya wanawake wakishakuwa kwenye mahusiano na mwanaume hujisahau kabisa na kupoteza touch.

Mwanaume anatakiwa awe na hofu ya mara kwa mara kama hutaki akusaliti. Lazima uwe updated na ujue vitu anavyovipenda ili kila siku akiwa mbali na wewe atamani mwanaume mwingine asiongee na wewe.

Unatakiwa umfanye mwanaume wako akufukuzie kila wakati wa maisha yenu, awe anahofia kukupoteza na ajihisi kuwa mshindi kwa sababu yuko na wewe.

Kwa kweli hapa kama hujajua ufanye nini ili jamaa yako aendelee kukufukuzia, basi fanya uchunguzi wako.

5. Usimdabidilishe

Hakunaga kitu kigumu kama kubadilisha tabia ya mtu. Kila mtu ana tabia zake tofauti, nzuri au mbaya. Wako ambao wanajitahidi kubadilisha tabia mbaya na kuchukua tabia nzuri lakini sio kitu kirahisi hata kama wao wenyewe ndio wameamua kujibadilisha tabia.

Ni rahisi kuhisi kwamba mtu anaweza tu kuacha ulevi lakini ni vigumu kwa mlevi kuacha ulevi.

Baadhi ya wanawake wanatabia ya kujaribu kubadilisha wanaume tabia zao kwa kuwakaripia, kuwapa adhabu, kuwanyima vitu vitamu, na hata kuwatenga. Hii ni njia moja ya kumfanya jamaa aanze kukuacha taratibu au akuone adui wa tabia yake.

Mpe sababu abadilishe tabia yake mwenyewe, na utumie ujanja na busara kumfanya aone umuhimu wa kuachana na tabia mbaya au ambayo unahisi haina manufaa kwake au kwenu nyote.

Hakuna kitu kibaya kama mwanamke anayetaka kubadilisha tabia ya mwanaume ili tu kujiridhisha yeye mwenyewe au kwa kuwa anaona yeye ndio yuko sawa na mwanaume wake hayuko sawa. Lazima utafeli.

Mwisho kabisa ni kwamba… Mwamaume na mwanamke wameumbwa na sifa tofauti ambazo zinahitaji kuunganishwa pamoja ili kupata ufanisi na maisha yenye furaha, lakini ni lazima watu hawa wawili wajuane na tabia zao ziendane.

Kama umepata kitu kipya kutoka kweney makala haya sio vibaya ukashare na mwingine, na kama una lolote la kuongeza tucheki kwenye Facebook na Twitter au email watupipo.com@gmail.com

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com