Nguo za mitumba zitatoweka mwaka 2018 au 2019?

Asilimia kubwa ya wananchi wa Afrika mashariki tumetumia second hand cloths kwa namna moja ama nyingine. Mpaka sasa mitumba ni mwokozi wetu kwenye maswala ya mavazi na hata kwa fashion pia.

A vendor sells secondhand cloths at a stall in the busy Gikomba market in Nairobi September 18, 2014. Shaded by ragged squares of canvas, amid choking dust and the noise of hawkers, shoppers in Nairobi’s Gikomba market can turn up Tommy Hilfiger jeans or a Burberry jacket for a fraction of the price in London’s Regent Street or New York’s Fifth Avenue. To match KENYA-TEXTILES/ Picture taken September 18, 2014 REUTERS/Noor Khamis (KENYA – Tags: BUSINESS TEXTILE)

Hili litabadilika miaka mitano mpaka kumi ijayo na pengine wakati huo wengi wetu tutakuwa na uwezo wa kuvaa nguo mpya (inshaalah)  bila kuumiza mfuko kwa kiwango cha standard guage.

Mwaka 2016 mwezi March Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi zilikubaliana kuzuia matumizi ya nguo zilizotumika katika soko la Afrika mashariki. Makubaliano ambayo tayari yameshaanza kuonesha usaliti.

Kwanini zinakatazwa?

Sababu za kuzuia matumizi ya nguo za mitumda ni pamoja na kuongeza soko kwa watengenezaji wa nguo wa ukanda huu, kwa kuwa soko kubwa kwa sasa limeshikiliwa na na wauza mitumba.

Ingawa kwa sasa Afrika mashariki haina uzalishaji wa kutosha kwa soko lake, serikali zote zimekubaliana kufanya mageuzi kwenye uzalishaji wa nguo na leather huku Rwanda ikionesha mwanzo mzuri.

Kenyans pick through second-hand clothes at the vast Gikomba street-market September 6, 2005. Despite widespread poverty across the east African nation of 32 million people, the last two decades have seen a roaring success in second-hand clothes trade known in local Swahili as “mitumba.” Shipped into Kenya in enormous quantities, vast piles of clothes are shifted at Gikomba, a teeming labyrinth of makeshift stalls, boxes, carts and barrows full of clothes and shoes in a densely-populate, pot-holed suburb of Nairobi. Picture taken September 6, 2005. REUTERS/Thomas Mukoya

Utekelezaji umefika wapi?

Rwanda imeongeza kodi kwa asilimia zaidi ya 1000 kweye nguo za mitumba ili kudiscurage biashara hii, huku serikali ikitoa ruzuku na kuvisaidia viwanda vidogo vya nguo.

Kenya mwaka huu wa 2017 ilitoa tamko kwamba haitaweza kuachana matumizi ya nguo za mitumba kwani bado uzalishaji wa ndani hautalitosheleza soko pamoja na export.

A man samples second-hand clothes (locally known as mitumba) at the Gikomba open-air market on June 25, 2012, in Nairobi. Local dealers welcomed Kenya’s Finance minister Njeru Githai’s move to lower import duty on ” Mitumba” in this year’s budget read two weeks ago. However, trade experts say the reduction on import duty, will put over 270,000 jobs in the cotton industry at risk and lives of farmers as well. AFP PHOTO/SIMON MAINA (Photo credit should read SIMON MAINA/AFP/GettyImages)

Push kutoka Marekani.

Marekani ndio nchi ambayo inaingiza nguo nyingi zaidi za Mitumba Afrika mashariki kwani biashara hiyo ina ukubwa wa kiasi cha $124 milioni kila mwaka.

Tangu kutoka kwa azimio hilo mwaka 2016 Marekani wamekuwa waki-lobby kujaribu kushawishi viongozi wa Afrika mashariki kutozuia mitumba na wengine kutishia kuzuia bidhaa za Afrika mashariki zinazouzwa nchini Marekani bila kodi kupitia soko la Agoa.

Sababu za Kenya kubadili mawazo

Wachambauzi wa masuala ya kibiashara wanadai kwamba kwa kuwa Kenya ndio muuzaji mkubwa katika soko hilo la Agoa, vitisho vya kureview makubaliano katika soko hilo yamefanya viongozi kusema kwamba hawako tayari kuzuia mitumba wakiogopa kukosa nafasi ya kuuza bidhaa Marekani. Je hili lina ukweli? Ntaendelea kukupasha.

Fursa kwa wafanyabiashara wadogo

Pamoja na yote yanayoendelea Afrika mashariki hivi sasa, wananchi tunapaswa kujua kwamba tuko kwenye wakati muhimu sana kiuchumi… Kila nchi kubwa inaangalia soko la Afrika mashariki kwa sababu ni soko linalochipukia kwa kasi na huku kukiwa na endless possibilities.

Ni wakati wetu vijana kuangalia fursa kubwa ambayo itaachwa na mitumba kipindi ambapo itazuiwa, move ambayo haitachukua miaka mingi sana kama ambavyo tunadhani. Je mafundi wa nguo wako tayari? Vijana wanaofanya biashara za kutengeneza nguo na fashion wameiona fursa hii inayojongea taratibu?

Nitaendelea kukupa stori za biashara na jinsi wana Afrika mashariki wanavyozichukua fursa zinazowazunguka.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com