Hutahitaji tena visa kutembelea nchi za Africa 2018

Ikiwa mambo yatakwenda kama yalivyopangwa… Mwaka 2018 swala la Visa kwa Africans wanaotembelea nchi nyingine za Africa litabaki kuwa TBT.

Kutokana na makubaliano baada ya African Union kuzindua visa ya Afrika, nchi nyingi zilianza kutoa visa on arrival ikiwa ni njia kuelekea kukomesha kabisa hitaji la Visa kwa wananchi wa Africa.

Namibia imekwenda mbele zaidi na hivi sasa serikali ya nchi hii inajaribu kuitisha muswada utakaopelekea sheria ya free visa kwa wananchi wote wa African countries.

Ikiwa nchi zote zilizoko ndani ya African Union zitasimamia utekelezaji huu wa kuondoa Visa kutoka kwenye nchi moja kwenda nyingine. Safari na ndoto ya kuwa na Africa kama nchi zitakuwa zimesogea zaidi.

Japokuwa wachambuzi wa maswala ya Africa hawanaoni mwaka 2018 kuwa mwaka wa kuanza kutumika visa moja tu kwa Afrika nzima… bado kuna matumaini ndoto ya kuiunganisha Afrika itatimia.

Passport yako ya Kenya au Tanzania inaweza ikawa haina maana kama unatembelea nchi za Africa.

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com