Ubongo wako ni wa ajabu kama unapata goose bumps unaposikiliza muziki.

Kila mtu ana namna yake ya kufurahia mziki. Wengine hufikia kulia wanaposikia baadhi ya nyimbo zinazowakumbusha nyakati Fulani katika maisha yao.

Lakini kwa wengi ambao husisimka na muziki kimyakimya huku mwili ukitoa vipele vya baridi na nywele kusimama dede, nyinyi akili zenu ni za kipekee.

Utafiti

Mwanafunzi wa zamani wa chuo kikuu cha Harvard Matthew Sach alifanya utafiti kupitia watu 20. 10 kati yao huwa wanapata msisimko na kutokwa vipele vya baridi wanaposikiliza baadhi ya ngoma na 10 ni wale ambao hawapati msisimko kwa kiasi hiki.

Katika utafiti huu Sach aliangalia activity ya Ubongo wakati ambapo watu hawa husikiliza muziki na kugundua kuwa akili ya mtu anayepata goose bumps wakati wa kusikiliza muziki huwa ni akili yenye nguvu na emotions nyingi zaidi.

Mapatikano

Findings za utafiti huu zimeonesha kwamba, akili ya mtu anayepata vipele hivi wakati wa kusikiliza muziki ina fibre nyingi na kuunganiska vizuri zaidi na sehemu ya auditory cortex na sehemu za ubongo zinazoleta hisia.

Nyakati ambazo mtu unaweza kusikiliza muziki na ukapata hisia kama hizi ni pale ambapo umesikia sauti ya msanii ikakugusa, lyrics nzuri, au mapigo ambayo huamsha hisia zako au kukukumbusha tukio la aina yake katika maisha yako.

Way forward

Unaweza kupata report ya utafiti huu wa Sach kwenye Oxfordacademic inayoitwa Brain connectivity reflects human aesthetic response to music.

Sach amesema ataendelea na utafiti huu kwa kuwa anaamini upo uwezekanao wa kutumia data hizi kutengeneza tiba ya matatizo kama depression.

Kama una lolote la kuongeza kwenye article hii nicheki kupitia Facebook au twitter Watupipo.com

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com