Ukifanya vitu hivi, vitakupotezea uwezo wa kusikia. Japo kimoja umeshakifanya.

Sikio na uwezo wa kusikia ni kitu muhimu sana. Hasa katika jamii ya Africa mashariki ambapo muziki wetu unakua kwa kasi. Ni vizuri ukaendelea kupata ladha ya muziki wetu.

Kuna mambo tunafanya kwa nia njema lakini yanapelekea kuharibu uwezo wetu wa kusikia.

Moja

Moja kati ya vitu tunavyofanya ambavyo vinaweza kusababisha ugonjwa wa masikio, ni style ya usafishaji kwa kutumia Q tip maarufu kama (ear stick, cotton stick, au pamba za masikio)

Dr Ana Kim ambaye ni mtaalam wa magonjwa ya masikio amesema, matumizi ya Q tip (pamba za masikio) husababisha kusukuma ndani vinyweleo vilivyomo karibu na ngoma ya sikio.

Vinywele hivi viko pembeni ya ngoma ya sikio, kwa ajili ya kuzuia uchafu na kuweka eneo la ndani katika hali ya unyevu unyevu. Vinywele hivi ni muhimu sana.

Mbili

Matumizi ya Q tip na takataka zingine zinazotumiwa mara nyingi mfano njiti za kiberiti, yanaweza kusababisha utoboe au ukwangue ngoma ya sikio (eardrum) na ukapoteza uwezo wako wa kusikia.

Tatu

Eneo la ndani la sikio ni eneo lenye ngozi laini sana. Ikiwa unaingiza vitu na kuchokonoa, unaweza kusababisha mchubuko ambao utasababisha infections za bakteria. Hii itakupa wakati mgumu, maumivu na pengine kupoteza uwezo wa kusikia.

Utasafisha vipi sikio?

Kama sikio lako halina ugonjwa aina yoyote, unapaswa kusafisha kawaida tu maeneo ya nje na mlangoni kabisa mwa sikio kwa kitambaa laini na maji safi kama unavyosafisha maeneno mengine ya mwili.

Sio lina mfumo wake wenyewe wa kujisafisha na ndio maana hutengeneza n’ta ambayo hutoka na kuanguka yenyewe.

Ikiwa ni lazima kusafisha ndani ya sikio, basi tumia bomba la sindano na maji safi yenye joto kiasi ambayo hayatakuunguza.

Ukijisikia hali sio nzuri siokioni, kuliko kuingiza vijiti, nenda kwa daktari atakusaidia bila kuacha madhara.

Acha mara moja

Kuingiza vitu vya ajabu ajabu siokioni, kama vijiti, njiti za kibiriti, funguo au aina yoyote ya vitu vigeni sikioni.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com