Uume wa jamaa umelika vibaya baada ya kutumia dawa ya Malafin kutibu malaria

Rafiki yangu tulipanga kuonana siku ya jumanne kwa ajili ya kufanya mishe zetu fulani. Iliofika mida ya ahadi akaniambia hajisikii vizuri atapitia Phamacy ili apate dawa ya kutuliza maumivu ya kichwa.

Tulikutana tukapanga kazi, ilikuwa tukutane siku inayofuata (Jumatano) ili kufanya shughuli zetu. Usiku wa Jumanne jamaa alinipigia simu akaniambia amezidiwa na anahisi kuwa ana malaria… Nikamshauri ni vyema akaenda kupima ili kujua kwa hakika kinachomsumbua.

Kesho yake nikampigia kumjulia hali, akaniambia anajiskia kupumzika maana kichwa kinamsumbua sana, na dalili za malaria… ikiwemo homa. Nikamshauri aende hospitali apate tiba then apumzike mimi nikaendelea na mitkasi.

Nilipopiga simu usiku wa Jumamatano kumjulia hali, akaniambia ametumia dawa aina ya Malafin ambayo ina mchanganyiko wa Sulfamethoxypyrazine na Pyrimethamine… Kwa kweli alikuwa anasound kama vile amezidiwa.

Kesho yake pia alikuwa anajisikia vibaya sana, lakini kuna mtaalamu wa afya alimwambia kwamba anajisikia hivyo kwa sababu ya dawa alizotumia, na kwamba angerudi katika hali ya kawaida.

Siku tatu mfululizo amekuwa akishinda ndani na anasema hali yake ya malaria imekwisha kabisa. Lakini amepatwa na tatizo lingine ambalo anahisi limesababishwa na dawa alizokula.

Tatizo lenyewe ni kwamba uume wake umechakaa kabisa sehemu ya kichwani. Na daktari aliyefika nyumbani kumtibu amemwambie kwamba dawa aina ya Malafin ndio imesabisha tatizo hilo.

Just kuweka ufahamu tena kuhusu dawa ya Malafin, ili kesho isije kukutokea na wewe. Dawa hii ina Sulfadoxine na pyrimethamine ambayo inaweza kusababisha madhara makubwa kwa mtu ambaye ana alergy na sulfonamide alergy.

Hata hivyo watu wenye matatizo ya figo hawatakiwi kutumia dawa hii.

Take care wakati unapotumia dawa ya Malaria bila kupima.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com