Mbinu tano za kufanya biashara yako ndogo, ishinde soko mbele ya kampuni kubwa.

Biashara ni mapambano. Ni vita. Japo sio vita ya kupigana, lakini kuna mazingira ambayo ni kufa au kupona.

Hebu fikiria, umefungua kibiashara chako kidogo, umekusanya ka-capital kako kwa miaka kadhaa. Lakini unapofungua tu biashara, unakuta kuna kampuni kubwa yenye mtaji mkubwa zaidi yako inafanya biashara kama ya kwako, na inatoa bidhaa kwa bei rahisi kuliko ya kwako.

Wateja wote wanaenda kwenye kampuni hiyo kubwa. Kila siku unaona dalili za biashara yako kufa. Utafanyaje?

Jibu liko kwenye stori ya mafanikio ya mfanyabiashara Joe Coulombe, na jinsi alivyoweza kushinda supermarket kubwa ambazo zilikuwa na mtaji zaidi ya supermarket yake.

Ilikuwaje?

Joe alianzisha maduka ambayo tunaweza kuyaita Mini supermarket mwaka 1967, wakati huo Joe alikutana na ushindani mkali kutoka kwa supermarket kubwa zilizokuwa zinafanikiwa kwa kasi za 7-11.

7-11 zilikuwa zina bidhaa nyingi zaidi ya maduka ya Joe na pia zilikuwa na mtaji mkubwa, hivyo bei ya bidhaa za 7-11 ilikuwa chini, kitu ambacho Joe hakuweza kushindana nacho.

Hatua ya kwanza – Change the game

Joe aliona kuwa vita hii asingeweza kushinda. Akafanya mapinduzi katika biashara yake baada ya kufanya utafiti na kugundua kitu ambacho 7-11 ilikuwa haina.

Kwa kuwa 7-11 ilikuwa na bidhaa nyingi na kwa bei rahisi. Joe akabadilisha mkakati na kuanza kuweka vitu vya hali ya juu na kubadilisha muonekano wa maduka yake. Vitu kama classy wine, goument foods nk.

Duka la Joe likawa la watu wanaopenda vitu special.

Hatua ya Pili – Re brand and upgrade

Sambamba na kubadilisha bidhaa, alibadilisha jina la maduka yake na kuita Trader Joe’s, na alihakikisha ana ajiri wafanyakazi wenye uwezo mkubwa katika kuuza. Alihakikisha anawalipa vizuri pia.

Joe aliwapa wafanyakazi wake uhuru wa kuhudumia wateja bila kufuata kanuni maalumu, na aliwahimiza wafanyakazi kuhudumu kila mteja kutokana na matakwa ya mteja na namna ambavyo mteja angependelea kupata huduma.

Hatua ya tatu – Motivation

Wafanyakazi walipewa motisha kwa kupandishwa vyeo ikiwa wangeonesha mafanikio katika utoaji huduma, na hata manager wa maduka yake aliwaita captains, ili kuwafanya wajisikie vizuri. Cheo cha captains kilikuwa kina mshahara mzuri sana, kiasi kwamba kila mfanya kazi alijitahidi kutoa huduma bora ili afikie cheo hicho.

Wafanyakazi katika kampuni ya Joe, walitengenezewa mazingira ya kuhudumia kama vile wanafanya kazi kwenye maduka yao wenyewe.

Hatua ya nne – Pay out

Hii ilifanya wateja wanaokuja kuhudumiwa kama watu special, kwa kuwa Joe alitengeneza mazingira ya wafanyakazi kujihisi wao ni special.

Hapo ndipo Joe alipoweza kufanikiwa kuinua kampuni yake ambayo ilikuwa imefinywa kwenye kona na kampuni yenye nguvu zaidi ya ya kwake.

Somo – Never give up, tafuta tundu lako

Leo hii kuna wafanyabiashara wengi ambao wanafunga biashara zao kwa kuwa wamefinywa na kampuni kubwa zenye mtaji mkubwa umaarufu mkubwa.

Stori hii ya mafanikio ya Joe, inakupasa ikurudishe kwenye ubao wa mawazo, kabla hujaamini kwamba umeshindwa, fikiria, ni kitu gani kinaweza kuwa silaha yako ya mwisho ya kukutoa kwenye kona hiyo?

Ukisubiri miujiza utafunga biashara, lakini ukituliza akili na kutafuta angle ya kipekee na ambayo inaleta maana kibiashara. Piga kama mshindi, utatoka.

 

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com