Usigombane tena na mpenzi wako kwa sababu ya hizi ishu.

Wakati mwaka unaishia ishia hivi, kuna wanaofurahia kuwepo kwenye mahusiano, wengine hawataki hata kusikia habari za kuwa na mpenzi. Wote mko sahihi.

Mapenzi yana changamoto. Hasa kama ni mapenzi serious, sio hizi habari za kudoweana. Ukiwa na mpenzi serious lazima mtakuwa na tofauti zenu… hizi hapa ni baadhi ya tofaut ambazo huwafanya wapenzi wengi kugombana.

Fedha

Kila mtu ana matumizi yake ya fedha. Unaokuwa na mpenzi halafu mkaanza kujaribu kutengeneza utaratbu wa kuumia pesa zenu mnazopata, huku mkipanga plans zenu za baadae, hii inaweza ikawa ngumu sana.

Mmoja anaweza kuwa anapanga kufanya kitu flani na mwingine anawaza kusave. Cha msingi ni kutuliza mifarakano na kukaa kama watu wazima na kuangalia ni jinsi gani kila wazo linaweza kufanyiwa kazi kwa nafasi yake.

Hamu ya sex iko tofauti

Kuna mmoja anaweza kuwa anapenda sana kurukiana, lakini mwingine sio kwa kiwango hicho. Unaweza ukawa na mpenzi ambaye kila siku anataka mfanye sex mpaka mchoke na kuchoka.

Katika mahusiano sex ni kitu muhimu sana, lakini pengine kufanya kila siku inaweza ikawa ngumu kwa mpenzi wako. Hapa sasa hatuwezi kuingilia. Endeleeni kutafuta suluhisho.

Jinsi ya kutumia muda wenu.

Kuna wakati huwezi kukaa na mpenzi wako kwa muda mrefu, lakini unakuta yeye anataka kuwa na wewe kila wakati. Sio kitu kibaya lakini ni kitu ambacho huwezi kufanya.

Rukia Sheba ametuambia kuwa wakati mwingi kwenye mahusiano ugomvi unatokana na kutotaka kuelewa upande wa pili wa shilingi. Anasema “wapenzi wanataka wao tu ndio wapate wanachotaka bila kuwafikiria wenzao”

Ingawa huyo ni mpenzi wako, muweke huru. Kama ametingwa na kazi, huwezi kusema acha kazi uje kukaa na mimi. Huo utakuwa mwanzo wa yeye kukuchukia.

Usafi

Hiki ni kitu ambacho at least kila mtu, ana kiwango chake. Kuna mtu kwake usafi ni sox kutokutoa harufu lakini mwingine usafi ni kutovaa sox mara mbili bila kuoshwa.

Katika mahusiano, hasa pale mnapokaa pamoja, ishu ya usafi ni muhimu sana kueleweshana mpaka kieleweke.

Utakuta wewe huwezi kuondoka kitandani bila kutandika na kuweka kitanda vizuri, lakini mwenzako akitoka hata mito anaacha imedondoka chini.

Utakuta mwenzio ni mtu wa kutupa sox au viatu kila kona ya nyumba, wewe ndio unakuwa ukihakikisha shajti halijawekwa kwenye dinning table.

Wengi hukutana na challenge hii na baadhi hugombana kabisa kutokana na suala la usafi. Je wewe na mpenzi wako mna challenge gani ambayo huwafanya mgombane?

Pamoja na challenges zote mlizo nazo. Dawa ya kwanza kuondoa tofauti ni kusikilizana. Sio kusikiliza tu bali kusikiliza na kuelewa mwenzako.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com