“Umejikwaa uka anguka na marafiki wanakucheka”. Hizi ndio SILAHA za kukuinua.

Tumekutana na kundi la vijana kijiweni hapa Dar esa salaam, wakipiga stori kuhusu rafiki yao ambaye, amepata hasara alipojaribu kufanya biashara ya kuuza nguo.

Kifupi, Hezron ni muuzaji wa mitumba ambaye ndio kwanza amepoteza mtaji wake wote, baada ya wateja wengi kukopa na kuchelewa kumlipa. Imefikia wakati hawezi kununua mzigo wa kuuza na pesa mfukoni pia haionekani.

Leo Hezron amekuwa kichekesho hapa kijiweni kwao kiasi kwamba aliamua kutoweka ili kukwepa kejeli na maneno ya dharau aliyokuwa anayapata toka kwa rafiki zake.

Sharif: Jamaa kuzungusha nguo kidogo tu akapotea kabisa kijiweni, ukajiona international artist tayari.

Marafiki: Hahahahahaa

Sharif: Mi nilijua haufiki mahali. Kuuza nguo sio mchezo, mtaji wenyewe wa kuunga unga. Haya sasa, leo hii yako wapi?

Haya ni baadhi ya maneno machungu toka kwa Sharif ambaye ni rafiki ndio muongeaji zaidi katika kijiwe hiki. Sharif yeye ni dalali na pesa zake anapata kutokana na kuongea.

Hii ni kawaida ya Sharif na genge lake. Wata mcheka muuza matunda, wata msimanga mpika chapati au mchoma nyama, na kum’beza mwimbaji anayechipukia kwa anapokosea, na leo wana m’beza rafiki yao kwa sababu wamesha jijengea mawazo ya kushindwa katika akili zao.

Unapokutana na marafiki wa aina hii, unahitaji kuwa imara sana ili usizame kwenye mawazo yao hasi.

Weka vitu hivi viwili mbele yako unapotaka kuanza biashara, ili usikate tamaa pale unapojikwaa na kuanguka katika biashara.

Challenges ni mafunzo na sio mwisho.

Hata unapokuwa shuleni na kuanza kusoma, unafundishwa jinsi ya kushinda challenges. Unafundishwa kuhesabu, unakosea tena na tena, mwalimu atakuchapa na kutumia mbinu tofauti mpaka uweze.

Hii ina maana umepewa challenge na ukaishinda. Japo haikuwa rahisi. Hata biashara yako haitakuwa rahisi… Utalazimika kutumia juhudu za ziada ili ufanikishe lengo.

Hivyo katika biashara, hata kama una idea nzuri na una amini itafanikiwa. Jiweke tayari kukabiliana na changamoto na sio ijiandae kusherehekea wa mafanikio.

Kama shuleni hukuweza hukujua kuhesabu vizuri siku ya kwanza uliyofundishwa, basi hata biasahara inaweza isifanikiwe mara ya kwanza. Pigana kufa na kupona kuhakikisha unafanikisha.

Tumia mbinu zote unazoweza kuzipata na usiangushwe na maneno ya kukubeza.

Jiamini. Hata wewe unaweza.

Confidence imezungumzwa mara nyingi na sote tunajua ni muhimu. Lakini unapofika wakati wa kuitumia confidence, hapo ndio vijana wengi hushindwa.

Kujiamini sio ishu ya kusema, ni kutenda. Sharif anasikilizwa na vijana wenzake na anapaza sauti kubeza jitihada za rafiki yake kwa kuwa yeye ameona ugumu. Hii ni kwa sababu yeye hana confidence ya kufanya anachofanya mwenzake. Japo moyoni mwake, anatamani angeweza.

Anatoa mifano ya watu waliofaulu kwenye biashara ya nguo kusema kwamba wao wamefanikiwa kwa kuwa wana hela, na kusisitiza kwamba ni imposible kufanikiwa kwenye hiyo biashara.

Kuna msemo vijana wengi wa Kitanzania wamekuwa wakiusema “Sio kwa Tanzania hii”

Msemo huu hutumika kusema kwamba, vitu vikubwa na vya kushtusha dunia haviwezi kufanyika Tanzania. Usemi huu huwavunja moyo vijana wanaojaribu pindi wanapokutana na changamoto.

Kwa kuwa binadamu hupenda kutafuta sehemu ya kulaumu linapotokea tatizo. Basi inakuwa rahisi kulaumu mazingira (Tanzania) pale mambo yanapoenda vibaya, na wanashindwa kujiuliza maswali ya kurekebisha makosa na kuboresha panapo hitajika.

Huu msemo ni mbaya sana katika maendeleo ya vijana wa Africa mashariki, na unapaswa kuufukia mbali na mawazo yako kama umeamua kufukuzia ndoto zako.

Happy Hunting endelea kupambana. No matter what FIGHT BACK!

pictures credits: Pinterest user. Huffington post.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com