Ishi ndani ya kipato chako 2018. Otesha pesa yako.

Mwaka umeisha. Tabia za mwezi December za kusherehekea na kuponda mali ndio zinaendelea hivi sasa. Sio mbaya.

Najua kuna baadhi ya watu ambao kila mwaka wanaweka mikakati kabambe ya mwaka mpya. New year’s resolutions.

Wengi mikakati hii husahaulika ndani ya miezi michache tu ya mwanzo wa mwaka.

Ili kuhakikisha unafanikisha mikakati yako ya mwaka 2018. Watupipo tunakushauri kuanzia na mikakati hii kwanza kabla ya kufikiria mambo mkubwa.

Acha kutegemea kipato kimoja

Kama unapokea mshahara, au unapewa pesa ya matumizi na mzazi/ndugu au jamaa. Fanya jitihada ya kufungua mlango wa pili wa kipato.

Unahitaji pesa ili kufanikisha mipango mingi katika, hata kama mpango mingine haihitaji pesa moja kwa moja.

Mfano, kama ni suala la kupunguza uzito, unahitaji kula haina fulani ya chakula, utahitaji kwenda gym. Kama huna pesa za ziada. Lazima kuna mahali utakwama.

Hivyo basi mwaka 2018, Fanya jitihada za kuongeza chanzo cha kipato chako.

Anza kutumia budget

Matajiri wote duniani, wameanza kutengeneza utajiri wao kwa kuishi kwa budget.

Usijidanganye kwa kuweka budget kali kwenye karatasi, halafu ukashindwa kuifuata.

Weka budget inayokiwezesha kuishi ndani ya wigo wako wa kipato. Ishi maisha unayoyamudu.

Kitu cha msingi hapa ni kuhakikisha unatumia kidogo zaidi ya unachoingiza.

Mwaka 2018, usiishi kwa kujilinganisha au kuvutia watu wengine.

Heri ya mwaka mpya.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com