Hizi hapa sifa 6 za mwaume ambaye siwezi kuolewa nae.

Baada ya maisha ya dating kinachofuata ni kufunga ndoa na kuanzisha familia. Boys wengi wa kisasa hamtilii maanani ishu ya maisha ya ndoa mpaka muda unapofika.

Well, kama una ndoto ya kupata mrembo akaingia kwenye ndoa na wewe lazima iwe na vigezo.

Watupipo.com imezungumza na warembo kadhaa jijini Nairobi, na hizi ndio sifa za mwanaume ambaye hawawezi kuolewa nae.

1. Mwanaume asiyejua kutumia pesa zake vizuri.

Girls wamesema, hawawezi kuwa na mwanaume asiyejua matumizi bora ya pesa zake.

“mwanaume anayeshindwa kupanga jinsi ya kutumia pesa zake kwa manufaa ya baadae, huyu sio mwanaume ninayemtaka”

2. Mwanaume violent

Kama kazi yako na sifa yako mtaani ni kuanzisha ugomvi na kupigana often, wasichana hawataki mtu kama wewe kwenye ndoa.

“Mtu ambaye anatatua mambo kwa ugomvi kila mara, au mtu ambaye hawezi ku-control hasira zake, siwezi kukubali awe mume wangu” mrembo Marian alituambia.

Girls wanataka mtu anayeweza kuwalinda, na kuilinda familia. Wanataka mtu anayeweza kupigana at least, lakini sio mtu mgomvi.

3. Mtu asiye na juhudi za kutafuta

Mrembo aliye tayari kuolewa hataki mwanaume asiyeweza kusakanya pesa. Wa kazi gani wewe?

Maisha ya sasa na huko tunakoelekea, pesa ndio kila kitu, hivyo mwanaume lazima uwe mchapa kazi. Unaweza ukawa na sifa zote nzuri, lakini kama huwezi kutafuta pesa, familia yako itaishije?

“Sichagui aina ya kazi, ili mradi ni kazi halali Mimi nitafurahi kuwa na mume anayefanya kazi na kuhudumia familia. Kama huna juhudi mimi sikutaki”

4. Mwanaume mwenye sifa za kijinga

Kuna wakati ni vizuri kuchukua compliments unapofanya jambo jema. Lakini mwanaume anayejisifia sana kupita kiasi, bila mpango, girls hawataki kumsikia.

So brothers, shusha kidogo majisifu kama unataka kupata make wa maana.

5. Mwanaume asiye na mipango ya familia.

Kuna baadhi ya wanaume kazi yao ni kufikiria starehe na maisha mazuri tu. Lakini kama mwanaume hana mpango wa maisha ya familia yake, hafai kuwa mume.

6. Mwanaume asiyeheshimu watu.

Ikiwa mwanaume haheshimu watu, hiyo hafai kuwa mume.

Itafika wakati familia inapewa lawama kwa sababu baba hana heshima.

“Siwezi kuwa na mume anayekosea heshima wengine, maana iko siku atanikosea heshima Mimi” alituambia mrembo mwingine anayeishi Nairobi.

All in all boys, hizi ni baadhi tu ya sababu zinazoweza kukukosesha mke. Japo ziko sifa nyingine unazotakiwa kuwa nazi, Fanya jitihada ya kujisafisha ili upate sifa za kupata mrembo wa maisha yako.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com