BANG! Hizi ndio tofauti kati ya Converse sneakers za wanaume na wanawake. Umevaa zipi?

Kutokana na watu wengi kupendelea viatu aina ya Converse, viatu hivi vimekuwa vikiuzwa kwa wingi duniani. Japokuwa vipo ambavyo ni Original na vingine ni fake, lakini pia vipo vya kike na vya kiume. Je utajuaje kuwa Converse hizi ni za kiume au za kike?

Kabla sijakuambia tofauti ya sneakers hizi maarufu zaidi duniani, chukua dakika chache kuangalia toleo hili jipya la Converse. Waterproof Converse ambazo zimetoka mwishoni mwa mwaka 2017.

Kati ya Converse hizi hapa chini, zipo za kike na kiume… Je utaweza kuona tofauti?

Tofauti kubwa katika Converse za kiume na za kike ni;

  1. Namba za Converse ni ndogo zaidi ya za kike. Mfano Converse ya mwanamke ikiwa namba 9, kwa mwanaume itakuwa namba 7 au 6. The same with kiatu cha no 12 cha kike ni sawa na namba 9 au 10.
  2. Kingine kitakachokusaidia kufahamu Converse ya male au female, ni rangi ya viatu hivi. Viatu vya kike mara nyingi huwa na rangi nzuri za kike na pengine urembo.
  3. Zipo Converse ambazo ni Unisex. Viatu hivi huvaliwa na wanaume au wanawake bila shida.

Cha msingi ni kwamba; Kuna tofauti ndogo sana kati ya Converse za kiume na kike. Ingawa hakuna tofauti katika material na ubora wa kiatu.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com