Usikae kizembe tena, sasa unaweza kusajili kampuni ndani ya saa moja tu nchini Tanzania.

Tulifanya mzungumzo na wafanyabiashara wadogo kutoka sehemu mbalimbali Tanzania na moja ya malalamiko makubwa ni ugumu wa kuanzisha biashara, hasa kwa upande wa kurasimisha (make it formal)

Walituambia kwamba, kijana anaweza kuwa na idea nzuri sana ya biashara na akaanzisha biashara, lakini linapokuja suala la kusajili kampuni, kupata leseni ya biashara, kupata usajili wa mamlaka muhimu kama TFDA, inakua ngumu sana kupata usajili.

Hivi karibuni yametoka matamko mawili ambayo yanaonesha kwamba serikali ya Tanzania inashughulikia matatizo na kujaribu kupunguza uzito kwa mfanyabiashara mdogo.

Tamko la TRA

TRA walitutangazia kwamba hivi sasa wanaanzisha mfumo wa kutoa grace period kwa wafanyabiashara ambao wanaanzisha biasahara.

TRA wamesema watatoa miezi mitatu kwa mfanyabiashara, kufanya biashara kabla ya kulipia kodi. Ilivyozoeleka ni kwamba, mfanyabiashara hufanyiwa makadirio ya kodi mwanzoni mwabiashara.

Tamko hili bado watupipo.com haijalifutilia kujua utekele

Tamko la BRELA

Lakini mamlaka ya usajili wa kampuni Brela nayo imetoa tamko kwamba kuanzia February mwaka 2018, wafanyabiashara wataweza kuanzisha biashara zao online na itachukua kiasi cha saa nzima kukamilisha.

Kutokana na mfumo huu wa kusajili kampuni online, haitakuwa lazima kwa mfanyabiashara kusafiri kutoka mkoani au nje ya nchi na kufika Dar es salaam kwa ajili ya kusajili kampuni. Kazi yote inaweza kufanyika kwenye mtandao ikiwa muhusika ana vigezo vyote vinavyohitajika.

Tanzania imewekwa iki kwenye nafasi ya 162 kati ya nchi 190 kwa nchi zenye urahisi wa kufanya biashara, kwenye rank za World bank.

Watupipo.com itazidi kufuatilia na kukusogezea vitu muhimu kuhusu hatua hii nzuri ambayo serikali imeweza kufikia.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com