Watanzania kunyweni maziwa basi, mtoe ajira kwa vijana na akina mama Kha!

Biashara ya maziwa na ng’ombe inaweza kuwa utajiri kwa vijana. Ikiwa kial mtanzania ataamua kuanza kunywa maziwa kwa hiyari yake na kwa wingi.

Katika hali ya kawaida kila mtu anatakiwa kunywa maziwa, kutokana na faida zake kiafya. Lakini watanzania wachahe sana wanakunywa maziwa.

Tanzania ni nchi ya pili Africa kwa kuwa na idadi kubwa ya ng’ombe huku nchi ya kwanza ikiwa Ethiopia. Hii inamaanisha kiasi kikubwa cha maziwa kinazalishwa lakini bado maziwa inaonekana kama luxury mtaani.

Hivi sasa Tanzania ni ya tatu kwa unywaji maziwa Afrika mashariki kwa makadirio ya kila mtu kutumia lita 45 kwa mwaka, huku Kenya ikiwa ya kwanza kwa lita 130 na Uganda ya pili kwa lita 80 kwa mwaka.

Kiwanda cha maziwa cha Tanga fresh kiliwahi kulalamika kwamba soko la maziwa Tanzania limejazwa na bidhaa kutoka nje ya nchi. Wauzaji hawa wa maziwa walilalamika kwamba kuna haja ya kupunguza uagizwaji wa maziwa kutoka nje, lakini tunaamini kwamba hata idadi ya wanywaji maziwa ikiongezeka kutakuwa na faida mbili kwa taifa.

Faida ya kwanza itakuwa ni afya ya watumiaji wa maziwa, lakini pia kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na mashuleni pia. Lakini pia wauzaji wa maziwa watapata fursa zaidi.

 

 

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com