Vitu 9 vya kipekee kwenye public transport jijini Nairobi aka Matatu

Kila mji una sifaa zake, ila kwa upande wa Nairobi public transport, nilishangazwa kuona hivi vitu kwenye magari ya abiria.

DJ ndani ya bus

Yes, yule DJ mwenye turntables na mixer utamkuta kwenye basi za Nairobi. Mfano Nganya (Matatu mpya mpya) zinazokwenda Rongai… dereva yuko mbele anachapa gia huku DJ yuko kwenye session.

Lipa zaidi kwa Matatu yenye mziki mzito

Mziki ni kitu muhimu sana kama unatumia usafiri wa public hapa Nairobi. Ni kama kuna disco. Matatu nyingi mpya na ziko Pimped vizuri, ni lazima ziwe na mziki mkubwa. Mkubwa kweli kweli hamsikilizani.

Kuna wakati nilipanda Matatu ina mziki mzito mpaka nilipofika safari yangu nikasikia njaa kali sana. Lakini hizi ndio gari ambazo zinacharge nauli kali zaidi. (Nchini Kenya hakuna kiwango maalumu cha nauli)

Nauli kubadilika kutokana na hali ya hewa

Ukiwa Nairobi kwenye Stage (kituo cha basi) halafu mvua ikaanza kunyesha. Automaticaly nauli inapanda saa hiyo hiyo. Hata kama dakika moja iliyopita ungepata gari ya Ksh30 utakuta imeshafika Ksh50.

Vitu vingine ambavyo huchangia nauli kubadilika ni idadi ya wasafiri. Mfano asubuhi na jioni nauli huongezeka na hasa kwa magari ya kisasa kama hili hapa..

Photo SDE

Screen kubwa na mziki mkubwa ina maanisha hii gari ni ya wenye hela. Kama huna kitu utapanda zile zee kabisa.

Hii mvua ikianza tu… ukiingia na kutoka umeacha mia… hata kama ulienda kusalimia mtu.

Kushuka ni kituoni tu

Unaweza ukapanda sehemu yoyote lakini kushuka ni kituoni tu. Abiria anaweza kusimamisha matatu hata Highway na ikasimama. Matatu za kwenda sehemu inaitwa Ngong kupitia njia ya Bypass… zinaweza kusimama na kupakia mtu Highway, lakini huwezi sema “Dere nishushe hapo mbele kama hakuna kituo” Unless dereva yuko na mood nzuri.

Konda ana haraka zaidi ya abiria.

Haya magari huwa na haraka muda wote. Hata abiria huyapenda kwa sababu ya kuwahi kufika. Hata kama wewe abiria huna haraka ya kuwahi hawa jamaa watakufikisha chap!

Zinaongoza kuvunja sheria njiani

Matatu ni kama vile zinamiliki njia. Sheria ya Kenya haicheki na gari inayo overtake, lakini Matatu hizi hazikaagi kwenye foleni hata kidogo. Wako radhi kulipa polisi ili waachiwe wafike haraka na kugeuka.

Matatu ikiwa haraka ndio bei inachangamka pia.

Bado wawili ijae… Na hakuna hata mmoja.

Utaingia kwenye basi na kukuta vijana kadhaa wamekuharakisha na kukuambia mtu mmoja au wawili wamebaki ili gari iondoke. Kumbe ni uongo mtupu.

Unaweza ukaingia kwenye gari na kukuta wanaume na wakati mwingine wanawake wamekaa kama wasafiri kumbe sio. Hawa huwa ni watu wa hapo stand ambao wanakaa ili gari ionekane imejaa, lakini akija abiria wanatoka mmoja mmoja.

Experience yangu na Matatu ni nzuri so far… Ukiacha siku moja ambayo nilikaa ndani ya Matatu ambayo ilikuwa full blast inapiga muziki wa Rock kwa sauti ya juu sana. Nikahisi kama nakwenda kuzimu kabisa.

Halafu TV kila kona. Huku nje huoni kutokana na mataa ya TV ndani ya gari, huku nje kelele zikisababishwa na utoboaji wa exhaust za gari kwa hiyo linapiga sana yowe.

Kuna maadhimisho ya utamaduni wa matatu

Hii sherehe hufanyika kushereheka utamaduni huu wa Matatu. Watu (hasa vijana) hufika kuangalia the best matatu na mshindi hupewa zawadi na taji.

Wifi bure

Karibu kila Matatu utakuta kibao chenye Username na password. Matatu Wifi lakini sio zote zinafanya kazi.

Wewe una experience yoyote ya Public transport ya kwenu? Je tabia za madereva zikoje, au tabia za kipekee za usafiri huko kwenu ni zipi?

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com