Listen Live!

Je unataka kurudi kwenye game baada ya kuwa kimya? Tumia huu ujanja alioutumia Nyashinski.

After Kleptomaniacs decided to take a break from music the name Nyashinski also disapeared from the headlines.
Baada ya kundi la Kleptomaniacs kuamua kupumzika muziki mwaka 2007, jina la Nyashinski pia lilipotea kwenye headlines.
Radio rotations pia kidogo kidogo zikasukuma ngoma zao pembeni as new HIT from other artistes came to the limelight.
Lakini tofauti na wasanii wengi wakongwe east Africa, Nyashinski haacha muziki, pengine alikuwa ameacha ku-perfom na kurekodi midundo mipya lakini alikuwa anafuatilia kwa ukaribu sana industry ya muziki.
“Ni kama vile mzae alienda kuchukua masters ili apande cheo kwenye kazi”
Maneno ya mtaani na kwenye recording studios yalianza kusema jamaa anarudi kwa kishindo. Sikuamini kwamba kishindo kitakuwa kikubwa kiasi kile.
Mwaka 2016 aliporudi na “NOW YOU KNOW” ndio nikamkabidhi heshima yake upyaa!
Leo hii Nyashinski anatakiwa kuwa somo kwa wasanii wa zamani kama akina Rey C, Juma nature na wengine ambao wanajitahidi kurudi kwenye game na kazi zao zinashindwa kupenya.
Usiharakishe kurudi kwa sababu vyuma vimekaza mtaani au umebahatisha kurekodi ngoma moja kali. Fanya utafiti mzito, tengeneza team ya kufanya ukirudi hauwezi kudondoka.
Post hii imekuwa Inspired na kilio cha dada yetu Rey C kuhusu muziki wa Bongo Flava na wasanii wa zamani.
Nyashinski pia anatufundisha kuangalia vizuri kujitathmini, na kujiweka juu sawa na thamani zetu.

 Utaitumiaje hii kwenye biashara?

Unaweza kuamua kubadilisha biashara au kupumzika kutokana na kukosa motisha au umeona hakuna maendeleo unayoyatarajia. Au pengine soko limebadilisha muelekeo.
Ruksa kuchukua sometime out na kujipanga.
But kumbuka unapofanya hivi unatakiwa urudi kwa kishindo ambacho kitakurudisha kileleni, ili uone thamani ya ile break uliyochukua.

You may also like...

WP2Social Auto Publish Powered By : XYZScripts.com