Ukitumia vyakula hivi ni sawa na tiba ya kubanwa na misuli.

Kubanwa na msuli ni moja kati ya vitu vinavyokera sana na wakati mwingine kuleta maumivu makali.

Zipo sababu za kitaalamu sana juu ya kwa nini misuli hubana, hiyo unaweza kuipata wakati mwingine.

Kwa sasa ukitumia vyakula hivi utapunguza tatizo la kubanwa na misuli;

Vyakula vyenye sodium

Sodium unaweza kuipata kwenye vyakula kama vile princles, na baadhi ya vyakula vya viwandani, lakini vi vizuri ukijitahidi kupata sodium kutoka kwenye vyakula vya asili. Hata maji ya bahari yanaweza kukufaa.

Vyakula vingine ni beetroot, celery, carrots, pesto, nyama choma na samaki choma , pamoja na olives.

Hii ndio misosi yenye sodium na inahitajika kwenye misuli yako.

Tumia vyakula vyenye potasium

Matunda kama melons (tikitimaji) citrus, Ndizi, Parachichi, mboga za majani, viazi, viazi vitamu, na maboga (pumpkin) pamoja na samaki.

 

 

Vyakua vyenye calcium

Calcium ni muhimu sana kwenye kutanuka na wepesi wa misuli. Unaweza kupata madini ya calcium kwa kutumia vyakula hivi, maziwa na dairy food nyingine, samaki wa kopo, dagaa wa aina zote, aina zote za karanga pamoja na mbegu tofauti tofauti.

 

 

Magnesium

Ni muhimu sana kwenye misuli, na inatumika pia katika kuzalisha nguvu.

Vyakula vyenye magnesium ni pamoja na maharagwe aina zote, parachichi, soybeans, mackerel, parachichi karanga mchele wa brown, cocoa dark chocolate na maziwa mtindi.

Wanasema kinga ni bora kuliko tiba na huu ni ukweli mtupu. Madini hayo yana kazi tofauti mwilini ukiacha kukuondolea muscle cramps.

Kama stori hii imesaidia please usisitte kutufuata kwenye kurasa zetu za mitandao au utupatie email yako tuweze kushare stori mpya kila zinapochapishwa hapa.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com