“Simu yako ya mkononi inavyo kuangamiza taratibu” – Danzel Washington

Audio blog post

Pale ulipo sasa hivi kuna aina ya simu ambayo unaipenda na wengi watakuambia kwamba iphone ndio the first choice kwenye market. Ukimpa mtu simu yoyote ile atachagua iphone.

Lakini rafiki yangu Rabii will differ with hiyo fact, na atasema Samsung ni chaguo bora. Ingawa wote wako sahihi kupingana kuna kitu kimoja ambacho wote wanaweza kukubaliana kwamba “Simu ni Mbaya”

 

Danzel Washington kutoka Whollywood anaamini kwamba jamii inaishi maisha ya hovyo kabisa.

Danzel : “Watu lazima waelewe, je unatumia simu yako au simu yako inakutumia?” Je unaweza kuzima simu yako na ukakaa vizuri tu kwa amani”

Danzel : “Unapokua unajua vitu vingi sana, basi utakua wewe ni mtu wa kupenda kuwa wa kwanza. Na utapenda kua wa kwanza mpaka hutajali kuwa mkweli tena”

Katika video hiyo Danzel anazungumzia madhara ya matumizi ya mtandao wa internet kiganjani kwa jamii.

 

Jamii kutengana.

Mahali fulani hivi sasa kuna marafiki ambao wamekwenda kula mahala, lakini badala ya kuzungumza na kusimuliana hadithi, wameshika simu zao na kupiga picha chakula na ku post mtandaoni.

Watu wanathamini zaidi kukubalika na watu wa mbali kiasi kwamba wanadharau uwepo wa watu wa karibu.

Unawaeza ukamwambia kitu rafiki yako aliyekaa pembeni na wewe lakini akashindwa kusikia, kwa sababu ameweka attention yake yote kwenye simu yake.

 

Watoto wadogo wanafundishwa kunyamaza.

92% ya watoto wadogo wa miaka 2 nchini Marekani, wanacheza video games. Je wanacheza saa ngapi?

Wazazi huwapa watoto simu ili kuwafanya wasilie lie, lakini watoto wanajifunza jinsi ya kuzitumia haraka sana.

Hii ni jamii ambayo inakuhimiza kuzungumza lakini mazungumo yote uyafanye online kimya kimya.

Na kwenye baadhi ya maeneo hata huko kwenye mtandao kuna mipaka.

Simu ni tatizo la psychology.

Simu ni kama vile kwenda faragha na aliyeko mbali. Je tumepoteza ile personal touch ya mtu wa karibu?

Matumizi ya simu ni suala la kisaikolojia, je tumepoteza ile desire ya kuwa karibu?

 

Asubuhi ni simu kwanza, mpenzi baadae…

Wengi huamka asubuhi na kukimbilia kuwasha simu na kuanza kuinteract na ulimwengu.

Umelala na mtu lakini akiamka badala akusalimie au akupige busu usoni, yeye ataingia online na kisha ndio akusalimie.

Je mtu wa pembeni yako au watu walioko mbali na wengine hawakujui, ni nani apewe attention zaidi?

Video hii inaonesha ni kiasi gani matumizi ya mtandao yanavyo sambaratisha utamaduni wetu.

Hakuna noma

Lakini kwa vijana wenyewe hawaoni tatizo kwenye ishu ya kutumia simu excessively la kutumia simu zaidi.

Wanasemekana ndio waathirika wakubwa wa matumizi mabaya ya simu za mkononi na mtandao.

Wanaongoza kwa kupotezea sauti zao halisi kwenye mitandao ya kijamii, mpaka inakuwa ni ngumu kumpata mtu real katika karne hii kwa sababu kila mtu anataka kuwa wa kwanza bila kujali ni halali au sio halali.

Bali kila kijana anatambua kwamba ana objective ya kujenga na kuimarisha uhusiano.

Cheki hii video taratiibu

You may also like...

WP2Social Auto Publish Powered By : XYZScripts.com