Top 5: Wizi mkubwa uliofanyika kiajabu sana na hakuna aliyewahi kushikwa.

6.6 Billion zilizopotea vita ya Iraq

Baada ya kumalizana na Saadam Husein, kiasi cha $6.6 zilipotea nchini huko na mpaka hivi sasa haijawahi kutajwa zilikopotelea.

Special inspector general for Iraq re-construction Stuart Bowen, alisema pamoja na jitihada zilizofanywa, mkwanja huo haujulikani uliko.

Mwizi aliyewatisha kwa bomu

Huko Japan, bank moja ilipatiwa kitisho cha kulipuliwa na bomu. Kitisho hicho kilitolewa kwa manager mkuu. Lakini baada ya ulinzi mkali kuanzia nyumbani kwa manager huyo mpaka ofisini. Siku ya tukio hakuna aliyelipuliwa.

Siku chache baada ya mambo kutulia, gari la kusafirisha pesa la bank hiyo likiwa limebeba kiasi cha $800,000 lilipigwa mkono na jamaa aliyekuwa amevalia nguo za polisi.

Jamaa waliposimama mtu yule akawaambia kwamba tishio lile la bomu limetekelezwa muda sio mrefu.

Akawaambia pia kwamba gari hilo ndio target ya pili ya shambulio hilo, walivyotazama chini ya gari wakaona moshi unatoka, wakakimbia na kumuachia gari yule jamaa… akalamba mkwanja kilaiiini.

 

Jamaa kaiba $200,000 kwenye ndege na kuruka

Jamaa mmoja aliyafahamika kam Dan ambaye baadae aliitwa DB Cooper, aliteka ndege aina ya Boeing 727 na kudai $200,000. Baada ya kupewa pesa hizo jamaa alilazimisha ndege hiyo kuruka kuelekea Mexico City.

Ndege ikiwa urefu wa 10,000 feet, jamaa akaruka na parachute. Miaka kibao imeshapita, haijawahi kujulikana kama jamaa alifanikiwa kushuka mzima, wala pesa hizo hazijawahi kupatikana.

 

$34 Million zilipoibiwa kwenye benki

Kundi la wezi lijulikanalo kama termites lilivamia bank kupitia mitaro ya chini ya ardhi (tunnels) nakuingia katika bank hiyo ambayo kwa muda huo ilikuwa imefungwa kwa ajili ya matengenezo.

Sasa jamaa wakatumia masaa kibao kuvunja na kuiba kwenye bank hiyo. Jamaa waliiba $34 Million na mpaka sasa hawajawahi kukamatwa.

 

Wizi wa bank kimazingaombwe

Kiasi cha $4 million ziliwekwa kwenye vault katika First National Bank, lakini watu walivyokwenda mapumziko ya weekend, jumatatu walikuta $1 tu ndio iliyobaki.

Inasemekana wizi huu ulifanyika kwa mazingaombwe kwa sababu hakuna alama zozote zilizowahi kuachwa kwenye wizi huo. Inasemekana mtuhumiwa mmoja alijulikana lakini hakuna mashtaka ambayo yamewahi kufanywa.

Mkwanja huo na wenyewe ulipotea tu kimaskhara hivyo.

Hizi ni tano za kimaajabu lakini zipo stori nyingine za wizi ambazo zimewahi kutokea duniani, na utaendelea kuzipata hapa watupipo.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com