Niliacha Kazi ya sheria na kuanzisha kiwanda cha kutengeneza Chocolate

Mjue Jaki Kweka: mwanamke wa kwanza nchini kuanza kutengeneza chokolate.

Kabla ya kuanza kutengeneza Chocolate nilikuwa nafanya kazi ya  Mwanasheria, lakini Idea hiyo ilikuja usiku mmoja tukiwa tumetoka  kupata chakula cha jioni na partner wangu wa biashara.

Tulikuwa na mawazao mengi ya biashara na mojawapo ilikuwa ni hilo la kutengeneza chocolate yetu wenyewe.

10962015_10152562836111540_390855387_n.jpg

Mwanzoni tulizungumzia juu ya kufungua aina fulani ya duka la kuuza chocolate nzuri zenye kiwango cha kukubalika na kila mtu.

Hata hivyo tuliangalia changamoto ya  kupata usambazaji wa juu wa kila siku hapa nchini. Tuligundua kunapengo kubwa la usambazaji wa chocolate nchini na pengo hilo linaweza  kujazwa na wazo letu na ndipo safari yetu ya ujasiriamali ilianza pale na tukaamua kuanza kutengeneza chokoleti yetu wenyewe.

Kutoka kuwa mwanasheria hadi mtengenezaji  wa kifahari wa chokoleti, lakini kabla ya hapo  siku zote nilikuwa nafanya vitu mbalimbali kama kutengeneza mikate ya kuoka na kuiuza sio kwa familia na marafiki tu bali kama biashara ya sideline wakati nikiwa nafanya kazi kama mwanasheria.

Kwa hiyo  haikua mabadiliko ya ghafla ingawa nilikuwa tayari nashauku ya kuifanya biashara hiyo na kufikia hatua ya kuwa imesimama vizuri.

Changamoto mbili kubwa nchini Tanzania kwa wafanyabiashara wengi hapa ni gridi ya nguvu ya upatikanaji wa mtaji kufanya mambo kama hayo .

Lakini changamoto nyingine ilikuwa inahusiana na chocolate yenyewe, kwa kuwa hakuna mtu mwingine Tanzania aliekuwa akitengeneza Chocolate na zote zilikuwa zikitoka nje inamaana ndizo watu walikuwa wamezizoea kutumia.

Kwa hiyo tulipokuwa tumeanza kutengeneza za kwetu watu kidogo walikuwa na mashaka nazo kutokana na kuonekana kutengenezwa locally, hatahivyo waliokuwa wanajaribu kuzila walizipenda na kuwa wateja wetu tunafurai kwa hilo,.

Kitu interestingly hapa Tanzania ni kuzidi kuongezeka kwa hitaji la bidhaa hiyo na pia kuuza nje cocoa kwa hiyo hii ni fursa nzuri kwa kila mtu.

Tunavutiwa kupata watu nchi za nje ambao wangependa kupata bidhaa zetu lakini bado sisi ni kampuni ndogo lakini tutafika huko muda sio mrefu.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com