Millard Ayo: “Hata mimi nimekosa mikopo mara 3″ Lakini ninaishi ndoto za maisha yangu”

Hii ni stori ya Millard Ayo ya miaka 8 kwenye industry ya media. Ameongelea kwa kifupi tu safari yake ya kuliagiza gari la kufanyia matangazo la @Ayotv na kusema kweli anastahili recognition.

Stori hii imefanya wengi tuhamasike kufanya yale tunayoyafanya kwa nguvu zaidi na watupipo wengi wame-react kwenye stori hii ya Millard.

Kwa wenye uwezo hiki kinaweza kuwa kidogo lakini kwangu ni kikubwa sana, mwaka 2010/11 nilipoanza kuwa blogger vitendeakazi pekee nilimudu kununua/nilivyokua natumia vilikua laptop ya laki 3 na simu ya Blackberry torch niliyoitumia kama camera. _ Leo namshukuru Mungu na kila binaadamu alieni-suport, nimepata gari ambalo ndani nimelitengeneza kama ofisi, litanisaidia kurahisisha kazi eneo la tukio kuliko awali na kurusha LIVE kutoka popote ambapo @vodacomtanzania wataniwekea Internet _ Hata hivyo haikuwa rahisi kulipata, ilikua ni ndoto niliyoiwazia sana miaka mitatu na nikaitimiza mwaka wa 4, huko mitaani najua viko vichwa, wapo wenye uwezo wa kazi na mipango ya maana kwenye kutafuta pesa lakini wamekwama kwa kukosa mtu wa kuwashika mkono au kwa kukosa vigezo vya kupewa mikopo, hata mimi pia nilikosa mikopo mara 3 Bank lakini baada ya kukosa mikopo ambayo ingetimiza sehemu ya ndoto zangu ndani ya miezi minne, nilikubali njia pekee ya kujikomboa ni kukusanya kila senti na nikaanza kufanya hivyo kwa miaka miwili na nusu mpaka nikapata pesa ya kununua hili gari nikamuagiza @drisaacmaro Japan na ninamshukuru sana kwa kunichagulia gari zuri _ Special Thanks kwa Maboss wangu CLOUDS @josephkusaga #RugeMutahaba, #Sheba na @sebamaganga kwa kuniruhusu kuishi ndoto zangu ndani ya ndoto zao, miongoni mwa pesa zilizonisaidia kwa kiwango kikubwa ktk kibubu ni zile za bonus ambazo Mtangazaji hupewa kipindi chake kinapofanya vizuri ktk mauzo, nina Brothers wengine WAWILI wa kuwashukuru SANA ktk hili, IPO SIKU YAO! _ Lilivyofika TZ nili-design muonekano wa nje kwa kushirikiana na @jukaytzeedream ambae ndie MCHORAJI BORA wa logo ya @ayotv_ , idea ya nje na setting ya ndani ilikuwepo nikalipeleka garage kwa my Brother Thabeet @tttrautoupgrades nako likakaa kama miezi minne naa… nilipopata pesa kulikomboa ndio nikalifata, kisha Fundi mwingine (Dani) akamalizia, nikikumbuka wengine nita-edit _ Nawakumbusha tu watu wangu tunaohangaika na hatuna wa kutushika mkono, anza na hichohicho kidogo ulichonacho haijalishi utachekwa au utaonekana umepoteza muelekeo, Asante kwa kila Mtanzania anae-support ninachofanya, naahidi kuyafanyia kazi mapungufu ili tupate bidhaa bora zaidi πŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏ

A post shared by millard ayo (@millardayo) on

 

  • vennyhappymackDuuh umeandika kitu ambacho ki uhalisia kimetujenga wengi…kwa akili ya kawaida ni rahisi kuwaza kwamba Millard huyu anaejulikana sana Tanzania na pengine nje ya Tanzania ana uwezo wa kupata anachokitaka kwa muda wowote anaotaka lakini kwa uhalisia kumbe hata wewe unazo ndoto zako ambazo unapata taabu kuzitimiza wakati mwingine ni kwa kukosa vigezo ambavyo wengine pia tunakosaga…pongezi nyingi kwako kwa hili na mengi tusiyoyafaham lakini zaidi pongezi nyingi kwa kutushirikisha mapito yako na kutuonyesha namna inavyowezekana.
  • markomota7Respect bro but the some times ss sote tunajifunza mengi kutoka kwako
  • omurangilakuna ishu naifanya ila vikwazo ni Vingi, nilishakata tamaa, ila hii post imenirudisha kwng mstar aisee, let’s hope tunaweza Mungu anatupigania basi na sisi tupigane kwa nafas yetu

    HII HAPA STROI YA MILLARD AYO NENPO KWA NENO

 

Kwa wenye uwezo hiki kinaweza kuwa kidogo lakini kwangu ni kikubwa sana, mwaka 2010/11 nilipoanza kuwa blogger vitendeakazi pekee nilimudu kununua/nilivyokua natumia vilikua laptop ya laki 3 na simu ya Blackberry torch niliyoitumia kama camera.
_
Leo namshukuru Mungu na kila binaadamu alieni-suport, nimepata gari ambalo ndani nimelitengeneza kama ofisi, litanisaidia kurahisisha kazi eneo la tukio kuliko awali na kurusha LIVE kutoka popote ambapo @vodacomtanzania wataniwekea Internet
_
Hata hivyo haikuwa rahisi kulipata, ilikua ni ndoto niliyoiwazia sana miaka mitatu na nikaitimiza mwaka wa 4, huko mitaani najua viko vichwa, wapo wenye uwezo wa kazi na mipango ya maana kwenye kutafuta pesa lakini wamekwama kwa kukosa mtu wa kuwashika mkono au kwa kukosa vigezo vya kupewa mikopo, hata mimi pia nilikosa mikopo mara 3 Bank lakini baada ya kukosa mikopo ambayo ingetimiza sehemu ya ndoto zangu ndani ya miezi minne, nilikubali njia pekee ya kujikomboa ni kukusanya kila senti na nikaanza kufanya hivyo kwa miaka miwili na nusu mpaka nikapata pesa ya kununua hili gari nikamuagiza @drisaacmaro Japan na ninamshukuru sana kwa kunichagulia gari zuri
_
Special Thanks kwa Maboss wangu CLOUDS @josephkusaga #RugeMutahaba, #Sheba na @sebamaganga kwa kuniruhusu kuishi ndoto zangu ndani ya ndoto zao, miongoni mwa pesa zilizonisaidia kwa kiwango kikubwa ktk kibubu ni zile za bonus ambazo Mtangazaji hupewa kipindi chake kinapofanya vizuri ktk mauzo, nina Brothers wengine WAWILI wa kuwashukuru SANA ktk hili, IPO SIKU YAO!
_
Lilivyofika TZ nili-design muonekano wa nje kwa kushirikiana na @jukaytzeedream ambae ndie MCHORAJI BORA wa logo ya @ayotv_ , idea ya nje na setting ya ndani ilikuwepo nikalipeleka garage kwa my Brother Thabeet @tttrautoupgrades nako likakaa kama miezi minne naa… nilipopata pesa kulikomboa ndio nikalifata, kisha Fundi mwingine (Dani) akamalizia, nikikumbuka wengine nita-edit
_
Nawakumbusha tu watu wangu tunaohangaika na hatuna wa kutushika mkono, anza na hichohicho kidogo ulichonacho haijalishi utachekwa au utaonekana umepoteza muelekeo, Asante kwa kila Mtanzania anae-support ninachofanya, naahidi kuyafanyia kazi mapungufu ili tupate bidhaa bora zaidi

 

Endelea kusimulia stori ya maisha yako unaweza kushare na sisi pia ili tukuhifadhie kumbukumbu zako hapa watupipo.com email us watupipo.com@gmail.com au watupipo.com on Facebook

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com