Unaweza kukosa mtoto kama mimi usipofanya maamuzi haya mapema. #Ladies

“Mwaka jana niliamua kufanya utafiti kujua kama ningeweza kuzaa mtoto mwenyewe bila usaidizi wa doctor. Nilipokwenda kwa daktari na kupima nyumba yangu ya uzazi, alishangaa sana na kuniambia kwamba ilikua inaonekana bado ni changa ukitofautisha na umri wangu. Akaniambia ninaweza kupata mtoto bila shida. Wakatai akinifanyia vipimo aliniweka kwenye mashine ya ultra sound ambayo ilinionesha nyumba ya uzazi pamoja na maelezo ya kutosha. Aliniambia ninaweza kupata mtoto. Moyo wangu unaendelea kupata maumivu kwa kuwa siwezi kupata mtoto, hivi sasa nina miaka 47. Lakini kila nikifikiria kwamba sina ndugu sina familia ambayo nina uhakika kwamba kwa lolote litakalotokea mtoto wangu atapata uangalizi mzuri. Niliamua kuendelea na mpango wangu wa kutokuzaa kutokana na sikujua kama mtoto atakuja katika mazingira gani. Inaniuma sana hili ndio shimo kubwa zaidi katika moyo wangu. Ninajuta kutokufanya jambo la uzazi mapema katika umri wangu. Ningeweza kupata mtoto nikiwa peke yangu tangu nikiwa mdogo lakini sasa ni too late. Nitajaribu kadiri niwezavyo kuishi sasa na sio kesho”

watupipo hii ni stori tumekutana nayo mtandao na kuona ni stori nzuri ya kushare na wewe… Niamdikie na wewe stori yako na kutuma kwa emai… watupipo.com@gmail.com au tuzungumze kupitia Facebook.com

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com