Housegirl huyu anafaa sana ila sitaki aendelee kufanya kazi hapa home. Mke wangu ni tufani

Hadi nimeamua kukaa cvhini na kuandika hivi ni uchungu mkubwa niliokuwa nao.. Roho yangu inanisuta sana.

Toka nimeoa ni muda sasa, mi na mke wangu tulifanikiwa kupata mtoto mmoja na hivyo tukaleta house girl atusaidie kazi mbalimbali. Huyu dada anatoka mkoa flani..Kiukweli ni mpole,mstaarabu anajali sana.

Anamwangalia mtoto vizuri.Mtoto akilia huyu dada atambembeleza kwa upendo sana na kumnyamazisha.Wife mtoto akilia huwa hataki hata kuhangaika kujua analia nini utasikia tu ” bupee….. Njoo umchukue mtoto mi nataka kupumzika” yule dada atamchukua mtoto na kumuuliza tatizo nini n.K

Kiukweli huwa inaniuma sana.Maana mtoto amemzoea na kumpenda housegirl kuliko hata mama yake. Hana habari na mama yake kama mama yake asivyo na habari naye.Nikiwepo mimi tutacheza vizuri n.K akiumwa anayejua kuwa mtoto anaumwa ni dada ndo atasema “Kaka leo xxx naona joto lipo juu” au leo anakohoa au ana mafua n.K. Nikisema twende hospital wife ananambia nimbebe mimi au twende na dada ndo awe anambeba.Yeye kucha ndefu hataki zikatike na amepaka rangi ya thamani sana.

Image result for mfanyakazi wa ndani

Lakini kwa unafiki huyu mke wangu ndo kwake.”Facebook na instagram zimejaa picha zake na mtoto akimwandika kwa majina mazuri ya kupendeza. Yaani utasema ana mapenzi sana kwa mtoto. Nikirudi toka kazini dada atanifungulia geti atakuja kunisubiria kama nina mizigo anipokee na kunambia pole na kazi. Wife hata akiwa likizo muda huo atakuwa sebuleni anacheck movie,anachat au yupo insta.

Dada ndo anajua tule nini,mtoto anakula nini,chakula kimeisha n.K niliumwa sana kipindi flani nakumbuka siku hiyo wote tupo sebuleni.Mimi na mke wangu.Nikatapika… Wife alichofanya ni kunambia nisitapikie kwenye sofa…

Dada alikuja akaniletea ndoo na pale chini akaanza kupiga deki.Matapishi yangu.Haraka akaingia jikoni na kuanza kutengeneza uji wa limao.Baada ya dakika chache nililetewa uji wa limao ninywe.Sikumwambia.Wife ameweka miguu juu busy na simu.Sikujua nimwambie nini.

Housegirl amelata uji ila anaambia ameniweka maji ya uvugu vugu bafuni nioge kwanza then nije ninywe uji nipate nguvu. Dawa alishazileta kaziweka mezani.Hali hii iliniuma sana….Maana haya ni mambo ambayo alipaswa ayafanye mke wangu.Nlijaribu sana kipindi flani kumwambia wajibu wake..Akanambia kwa dunia ya sasa wote tunafanya kazi so ni ngumu naye anarudi amechoka..Ningetaka mwanamke wa hivyo ningeoa ambaye ni mama wa nyumbani.

Related image

Kuna mengi ambayo sitaki yaelezea. Na niwe mkweli huyu dada hajaonesha hali yoyote ya kunitega. Anafanya from the heart. Na malezi ya mtoto naona hata mtoto mwenyewe anampenda sana dada kuliko mama yake. Na mama yake proudly kabisa nimemsikia akizungumza mbele ya wenzie “Yaani xxx mimi nikiwepo wala hajali ye kila wakati tu ni aunt aunt… Kama vile mimi sipo… Mi namwachia aunt yake si namlipa? Ndo amwangalie mtoto wangu vizuri sasa” nliumia sana.

But nimewaza haya baada ya kuona huyu dada anaingia moyoni mwangu.Aliishia form 2 ila she is so smart.Ana akili na anajua kuishi na watu. Nimejikuta naanza kumpenda.Napomtizamana najikuta mapenzi yananivuta kwake.

Mara kadhaa namtizama najikuta moyo unashtuka.Nawaza why sikumwoa yeye? Mwaka wa pili naishi naye mtoto anakua mikononi mwake akiwa na afya njema kabisa. Ana mapenzi kwa watoto, ananijali ananiheshimu. Mke wangu ana sura na umbo zuri.Ila ni mjeuri,mkaidi mwenye majivuno na dharau kwa watu.

Image result for mfanyakazi wa ndani ananivutia

 

Nataka nimwondoe house girl maana mapenzi yananizidi kwake. Nami sitaki kufanya kosa la kutembea na house girl.Sitaki nimwaribie na yeye..Ila nawaza nikimwondoa ntamwondoa kwa sababu gani.Hajanikosea kitu? Then mtoto atakuwa katika hali gani?Maana mtoto anampenda sana aunt yake. Sana kiasi kwamba napata shida ataishi vipi na je ataathika kiasi gani?Nitamwambia mke wangu kwa nini tumwondoe?

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com