Msomi mwenye Degree aliekataa kuajiriwa na kuwa mbunifu wa mavazi.

Anaitwa Jacquline Magayani Mwenye taaluma ya habari ambaye alikataa kuajiriwa na kuamua kuwa mbunifu wa mavazi.

Alianza kuuza nguo kawaida ila baadae alitaka kuuza nguo zenye logo yake mwenyewe basi katika kurealize ndoto yake akafata mzigo China mwaka 2013.

Lakini bahati mbaya aliibiwa pesa zote ambazo ndo ulikuwa mtaji wake basi kwa crisis aloipata akaamua kurudi nyumbani kujipanga upya hakukata tamaa.

Baada ya muda akaona kwanini tu asianze kuuza nguo zake ambazo atadesign mwenyewe basi ndo akaanza na fundi mmoja mwaka huo huo na sasa wako mafundi zaidi ya sita.

 

Jacquescollection-27

Anasema alipoona pia kuwa african prints zina trend sana akaona aanze na vitenge kudesign na kushona.Wakati huo alikuwa Jijini Dar es Salaam, Mwenge na baadae kuhamia  Mwananyamala.

Jacqueline ni msomi mwenye digrii ya uandishi wa habari ila hajawahi kupractice yeye alianza ujasiriamali kitambo hakutaka kuajiriwa.

Jacquescollection-20

 

matarajio yake ni  Kuwa na ofisi kubwa zaidi ambayo itakuwa na section mbali mbali pia anataka atengeneze nguo readymade mtu asije tena kuanza kudiscuss nini anataka kushonewa aje tu na akute nguo tayari  yeye anunue tu.Anampango wa kugrow zaidi nakuwa na website yake ili kuongeza trust yake kwa wateja.

Jacquescollection-23

alifanikiwa ku launch collection yake aliyoipa jina la Moyo Safi ikiwa inafocus kwa matatizo yake aloyapata kuonyesha jinsi gani amerecover na hakukata tamaa .

ili kuweza kujitangaza  Jacqueline aliamua kufanya biashara yake kupitia mitandao ya kijamii kama  etsy.com,pinterest ,insta na facebook pia  anadisplay designs zake na kuchukua order za wateja wake,pia anapost wateja watakaopenda kupostiwa kuonyesha au kushare nguo walizodisainiwa na Jacqueline.

 

Jacquescollection-34

 

 

 

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com