Niliacha kazi Benki na Kuuza Nguo Nikafanikiwa.

Biashara ya nguo ni moja ya masoko ya kuvutia sana na makubwa zaidi katika bara la Afrika. Pamoja na idadi ya watu zaidi ya bilioni 1, na inatarajiwa kufika mwaka 2050 itakua ni bilioni 2.2 , ukuaji wa mavazi ya Afrika na sekta ya mtindo itakuwa kubwa kwa miaka ijayo.

Hivi sasa,  sekta ya mavazi ya Afrika inategemea uagizaji kutoka nje ya nchi. Hata hivyo, inaleta furaha kuona  idadi kubwa ya wajasiriamali wa Kiafrika wanaingia ndani ya soko kwa kutumia miundo iliyopatikana ndani ya nchi na kukidhi ladha ya kipekee.

Image result for CLOTHING COMPANY

Llyord Martin ni mjasiriamali na mwanzilishi wa Fow clothing line ambayo iko Marekani na kirefu cha Flow maana yake ni “Future Leaders Of the World”.

Kabla ya kuanzisha biashara yake ya nguo alikuwa  akifanya kazi katika benki moja lakini aliamua kuacha ili  kufuata hamu yake ya  kuwa mjasiriamali.

Image result for AFRICA CLOTHING WORKSHOP

Anazungumzia mengi juu ya shauku na kuhakikisha kuwa nguo zake anazotengeneza zinakidhi mahitaji katika soko na pia kufanya biashara hiyo sio kwa lengo tu la kujipatia fedha bali kuwa mvumilivu kwani kupata faida kubwa inategemea na mchakato wa muda mrefu baada ya kutengeneza njia.

Lakini kikubwa zaidi anadai kuwa kabla ya kufanya biashara hiyo ni lazima kwanza mjasiriamali afanye tafiti juu ya uhitaji na aina ya nguo zinazohitajika katika soko na kufanya kazi kwa nguvu zote.

Watu wengi wanatafuta njia za mkato ili kuanza lakini Lloyd anasema “ni upumbavu kujijaribu katika mchakato wa kujifunza.”.

Image result for AFRICA CLOTHING WORKSHOP

Jambo lingine muhimu ambalo anazungumzia ni kuendeleza mpango wa mauzo. Kwa ushindani mkali katika sekta ya mavazi, kila mjasiriamali ambaye anatarajia kufanikiwa katika sekta hii lazima awe na mpango wa kukuza soko lake na kuuza nguo zake.

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com