“Mistakes nne ambazo hutakiwi kuzifanya ukiwa kwenye mahusiano”

Kuishi na yeye bila ndoa

Hili ni kosa sitarudia katika maisha yangu. Mwanaume alinichukulia poa sana baada ya kuanza kuishi nae wakati hata nyumbani kwetu hawakua na habari.

Kumpa hela

Mwanaume nilihangaika kumtoa out na kumletea zawadi kila nilipoweza. Kumbe huku yeye anatumia hizo pesa akabweteka na hata kazini ameanza kuzembea mwishowe nikahisi ameacha.

Huyu mwanaume alifikia wakati akawa anatumia hizi pesa zangu kuhonga mtu mwingine.

Kumsamehe baada ya kusaliti

Jamaa alikuwa na uwezoo wa kunipa vitu vya kipekee. Siku niliyodundua anatoka na mtu mwingine niliumia sana. Lakini baada ya hasira kuisha na maombi mengi ya msamaha huku akiahidi hatarudia tena; mimi nilimkubalia.

Kumbe hakuna lolote ni maumivu tu.

Kupokea zawadi za ex wake

Kuna wakati alikuja na hereni nzuri sana, lakini akaniambia kwamba alikuwa amemnunuliaga ex wake na alitaka mimi nizichukue.

 

Nilikubali kuvaa hii cheni lakini leo najua ilikuwa ni mistakes sana.

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com