Kwa nini niliacha kazi na kuanzisha biashara ya kuhifadhi bidhaa inayonilipa zaidi.

Miaka minne iliyopita, Njeri Wainaina alijikuta asiyekua na furaha  na kazi mbili ambazo alikuwa amefanya. Alikuwa akifanya kazi kama afisa masoko na mahusiano ya umma. Akiwa na umri wa miaka 24, aliamua kuachana na ajira kwa ajili ya mradi wa ujasiriamali. Kwa Sh5,000 tu za Kenya mwaka  2015, aliiandikisha kampuni yake, Uwakala ya  Wachia, na kufungua  biashara yake.
Alianza kusambaza  bidhaa za jumla kwenye mahoteli na vituo vingine na taasisi. Hata hivyo, alihisi kwamba hakuwa akifanya vya kutosha kuishi kulingana na uwezo wake, na hakuweza kutingisha hisia kwamba mstari wa biashara aliyokuwa akifanya  haikuwa endelevu.
“Nilitambua ajira haikunifaa na kuanza biashara yangu, lakini bado sikuwa na furaha,” anasema. Kuanza Wakati akifanya shahada katika mawasiliano na mahusiano ya umma katika Chuo kikuu cha Ufundi cha Kenya mwaka 2013, Njeri alikuwa ameanzisha mpango mkakati wa biashara ya ndoto zake.
Hakuzindua biashara yake hiyo toka mwanzo akiwa na wazo hilo kutokana na kutokuwa na mtaji utaowezesha ndoto yake kuwa kweli. Lakini miaka mitano baada ya kuandika na kupannga wazo lak alikuwa na hisia katika sekta ya vifaa, alijua hawezi kuendelea kupuuza hilo.
Image result for storage space
Aliamua kuanza tu na kile alicho nacho. Baad ya muda mfupi, Njeri hatimaye alijua alikuwa akiishi ndoto yake baada ya kuanzisha kitengo cha kuhifadhi bidhaa kwenye Mitaa ya Koinange iliopo  Nairobi Kenya. Anatoa huduma kwa wateja ambao wanataka bidhaa zao kuhifadhiwa kwa muda mfupi.
“Nilikuwa na shauku kubwa kuhusu biashara hii tangu nimekuwa na wazo wakati nikiwa  chuo kikuu. Ni nini kilichochochea mimi kufikiria kuhusu ujasiriamali. Nilihisi kuwa itakuwa hatua kubwa ya kufungua fursa mpya za ukuaji kwa ajili yangu, “anasema.
Image result for storage space
Wakati Njeri ikipanga mpango wa biashara hiyo mwaka 2013, Biashara kwa njia ya mtando ilikuwa inajulikana kwa  watumiaji wa mitandao wa Kenya, na biashara za mtandaoni zilikuwa zinakuja juu kwenye vyombo vyote vya kijamii.
Image result for business online
Kwa Njeri, swali hili ambalo lilimfufua, ni wapi wafanyabiashara hawa watahifadhi bidhaa zao wakati wa kusubiri wateja waweze kuichukua kutoka katikati ya Mji, Na kwa wale wanauza nguo, wapi wateja wao watajaribu kuwapata?
“Nilikuwa na marafiki ambao wanafanya  biashara za mtandaoni. Walikuwa wakiuza bidhaa za urembo, nguo na viatu, na nilikuwa na ufahamu kwamba hawakuwa na sehemu ya wateja wao kuweza kupata bidhaa hizo, “
Image result for beauty products storage space
 Muda mchache wazo lake lililoanzia chuoni, liliweza kumuajiri na  kuajiri wafanyakazi wengine kadhaa na katika ndoto zake zijazo alitaka kuendelea kukuza biashara hiyo na kuongeza store nyingine nyingi katika Mji wa Nairobi na wilaya zake.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com