Wajue wajasiriamali waliofanikiwa 5 ambao waliacha kazi zao na kufata ndoto.

Wengi wetu tuna ndoto za kuwa huru Kifedha kujitegemea na kuondoka kwenye stress za ajira lakini bahati mbaya walio wengi hawana ujasiri wa kuthubutu na hatimae kushindwa tunachotaka kufanya

Wajasiriamali wafuatao walifanya maamuzi ambayo yanaweza hata wewe Kukupa matumaini yanayoweza kubadilisha fikra yako na kujifunza kupitia wao.

Wengine wamekuwa wakiogopa na  badala yake kuruhusu sauti za kukatisha tamaa, wajasiriamali wafuatao chini wao waliamini kuwa  wanaweza kufanya chochote ambacho wanafikiria kichwani.

Hapa kuna wajasiriamali waliofanikiwa 5  ambao waliacha kazi zao ili kufuata shauku zao. Haujachelewa  sana na ndoto hiyo bado unaweza kuifikia. Unahitaji tu kuona na kutendea kazi.

1. Ben Kiruthi – Mpigapicha maarufu alieshinda Award Afrika.

Image result for Ben Kiruthi – Award Winning Photographer

Ikiwa mtu yeyote anaweza kukuambia kuwa mpiga picha huyo alieshinda tuzo alikuwa ni mhandisi, labda unaweza usiamini.

Akiwa kijana, Kiruthi alisomea taaluma ya Uhandisi na ili kuwa mpiga picha ni lazima alikuwa akihitaji juhudi kubwa.

Baada ya kumaliza chuo aliajiriwa kama mhandisi aliekuwa akilipwa kiasi cha Ksh 30,000 kwa kila mwezi.Hata hivyo sio kitu alichokuwa akikitaka kufanya katika maisha alitambua hilo.

Aliamua kuwa interest na kupiga picha .Yeye pamoja na mke wake walipata changamoto katika kujifunza kwa juhudi kupitia mtandao wa YouTube na kufanya majaribio ya kupiga picha nzuri.

Na sasa kwa maamuzi yake ya kuacha kazi amejijengea ngome imara ambapo anatengeneza fedha kiasi cha Ksh 500,000 kwa mwezi.

2. Gloria Michelle Otieno – Mkurugenzi wa  Recours Four Kenya Consultants

Image result for Gloria Michelle Otieno – CEO Recours Four Kenya Consultants

Gloria Michelle OTitieno alikuwa akifanya kazi katika shirika la ndege la Kenya katika kitengo cha kuhudumia wateja lakini aliamua kutoendelea na kazi hiyo ambayo ilikuwa haimridhishi.

Alikuwa anafanya kazi hiyo bila kuwa na mapenzi nayo lakini alishauri kuwa sio kila mtu anayechukizwa na kazi yake basi ni lazima aiache lakini awe na plan B.

Mteja wake wa kwanza alikuwa ni kijana mwenye umri wa miaka 22 aliemwandikia CV kwa Ksh 200 na baadae alimwandikia tena cover letter kwa Ksh 150 baada ya kuridhishwa na CV nzuri.

Na hapo ndipo ilikuwa mwanzo wa safari yake na kuanza kuwa mshauri kupitia kampuni yake ya Four Kenya Consultant.

3. Wambui Mukenyi – Mbunifu wa mavazi.

Related image

Huyu alijifundisha mwenyewe kazi hiyo ya ubunifu wa mavazi alikuwa na nguo za kifahari za Afrika ambazo zilikuwa zikivaliwa na matajiri na kuona kuwa ni fursa kubwa kwake kuanzisha biashara bubwa.

Alifanya kazi kama muhasibu kwa miaka miwili katika kampuni ya kutengeneza Muvi lakini alijiona kama yupo mahali asipostahili.

Baadae aliona aache kazi yake na kujidhatiti katika ubunifu wa mavazi muda wake wote.

Nakutokana na maamuzi hayo alifanikiwa kuwa anawavalisha watangazaji maarufu wa luninga kama NTVs,  Victoria Rubadiri, Lilian Muli, Janet Mbugua pamoja na Kambua Manundu.

Na saivi amekuwa mbunifu wa mavazi maarufu ambaye hajutii kuacha kazi yake na kufata ndoto yake ya muda mrefu.

4. Kevin Kairuki

Image result for vegetable delivery

Huyu kijana mdogo anavutia kila mtu ambaye anataka kutengeneza maisha vizuri wakati akiwa bado kijana.

Mjasiriamali huyu mdogo alianza na kiasi cha Ksh 5,500 ni wangapi kati yenu mngeweza kufanya hivyo.

Sasa alikuja kuwa na biashara yake ya Blessed Basket akifanya kusambaza mbogamboga pia kutengeneza Keki na kufanya  event planning business.

Wakati akihojiwa na Daily Nation alikiri siku biasharayake ikiwa mbaya huingiza kiasi cha 100K.

5. Dr. Muhoro Muriithi Paul – Mmiliki wa  Charlie’s Bistro

Image result for good restaurant

Ukilisikia jina lake lilivyokuwa maarufu unaweza kudhani kuwa ni mtu wa makamo sana  lakini kumbe ni kijana wa miaka 32 ambaye ndio mmiliki wa mgahawa wa Charlie Bistro, restaurent matata sana iliopo katika Junction ya njia ya Mbagathi na barabara ya Lan’gata  na pia hufanya biashara nyingine za hapa na pale.

Huyu aliasha kufanya kazi yake ya taaluma ya madawa ya binadamu na pia ni mtu ambaye alikiri kutojutia maamuzi hayo.alidhani kuwa alipenda medicine lakini aligundua kuwa biashara ndio iliokuwa ikimuita zaidi.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com