Zijue faifa za kula Wadudu.

Inakadiriwa kwamba kufikia mwaka 2050, idadi ya watu duniani itafikia bilioni tisa.

ili kuweza kupata vyakula vya kutosha idadi hiyo ya watu , itabidi uzalishaji wa chakula uongezeke maradufu.

Idadi ya watu duniani inapopanda, kuna juhudi za kutafuta njia mbadala za kupata chakula – hasa protini – badala ya vyakula vya kawaida kutoka kwa mifugo na samaki.

Kula wadudu ni moja ya njia hizi mbadala.

 

Image result for senene

Hili linasifiwa sana kwani wataalamu wanasema ni endelevu kimazingira, wana virutubisho vingi na wanaweza kupatikana kwa urahisi, kwa gharama nafuu na katika hali nzuri.

Maanufa ya kula wadudu

Wadudu wanaweza kuliwa na vyakula vingine, mfano pizza

“Wadudu ndio chakula halisi chenye virutubisho karibu vyote.

“Wana protini, madini mengi na asidi za amino na kwa hivyo ni faida sana kuwala.”

Wadudu pia huwa bora kwa mazingira ukilinganisha na ufugaji.

Image result for bee cooked

 

Wanaweza kula taka, hawatoi gesi zinazochangia ongezeko la viwango vya joto duniani, hawahitaji maji mengi na huhitaji eneo kubwa la shamba kuwafuga.

Wadudu pia wana kiwango cha juu sana cha kubadilisha mali ghafi kuwa kawi au chakula kwa sababu hawahitaji kudhibiti joto katika miili yao kwa kutumia damu kama wafanyavyo mifugo na wanyama wengi.

Kwa kawaida, wadudu wanaweza kubadilisha kilo 2 za lishe kuwa sehemu ya mdudu.

Ng’ombe atahitaji kula lishe ya kilo 8 ndipo aweze kuongeza kilo 1 katika uzani wake.

Ni wadudu wa aina gani wanaoliwa?

Kuna karibu wadudu aina 1,900 ambao wanaweza kuliwa duniani, kwa mujibu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO).

Wengi wa wanaoliwa ni mende, viwavi, nyuki, nyigu, nzige, kumbikumbi, nge, vipepeo na kerengende.

Image result for eating cockroaches cooked

 

Licha ya kwanda wadudu hawa wanapatikana kwa wingi, ni aina chache sana ya wadudu hawa wanaoliwa na jamii Afrika Mashariki.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com