Jinsi ya Kudhibiti Stress Katika Biashara.

Hatua ya Kwanza

Ni kuielewa kuwa huo msongo wa mawazo unatokana na nini, Kwa hivyo chukua kalamu na karatasi uandike, labda inatokana na kazi nyingi sana zimerundikana au kuna kazi ambayo ulitakiwa kuikamilisha ndani ya muda fulani lakini muda unakaribia kufika na bado hujamaliza.

Image result for plan job work

Ukishajua  stress yako inatokana na nini, na ushaandika. Kwa mfano stress yako inatokana na kuwa una kazi

nyingi na unatakiwa kuzikamilisha ndani ya muda husika. Unachotakiwa kufanya ni kuandika kila kazi/project na mwisho wake (lini inahitajika). Kwa mfano Kazi ya kwanza inatakiwa baada ya siku 5, kazi ya pili inatakiwa baada ya wiki 1.

Hatua ya Pili

Fanya kitu kimoja kwanza mpaka umalize ndipo uende katika kazi nyingine. Kwa mfano katika kazi ulizonazo

kuna kazi unayotakiwa kuikamilisha  baada ya siku 5. Anza na hiyo kazi na usifanye kazi nyingine mpaka hiyo

ikamilike.

Related image

Hatua ya Tatu

Jiulize, Nifanye nini ili niweze kumaliza hii kazi/project haraka na nani ninaweza nikamtafuta ili anisaidie

nifanye hii project haraka. Muda mwingine unahitaji mtu wa ziada wa kukusaidia kutatua tatizo lillilopo,

usibebe mzigo peke yako, unaweza hata kumchukua mtu kwa kumlipa.

Related image

Kama umejikuta  kila mara unapata stress katika biashara yako basi wewe umekuwa unaendeshwa na watu.

Ili kuepuka hilo Tenga muda usiku au hata asubuhi mapema weka ratiba ya siku yako, kwamba leo  nitafanya

hiki na hiki na usiruhusu mtu kuharibu ratiba yako labda kuwe na dharura kubwa iliyojitokeza. Kwa kufanya

hivyo itakusaidia sana kuweza kudhibiti msongo wa mawazo na kuendesha biashara Yako Vizuri.

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com