Mitumba, maua na mito vilivyomnyanyua Evely

Wakati wengi wakiwa wanajihusisha na biashara za kawaida kama vile kuuza vyakula na biashara ndogo, wapo wengine ambao wamekuwa wakifanya biashara kubwa.

Hata hivyo, wanawake wanaofanya biashara hizo kubwa, wengi walianzia kwenye biashara za kawaida, lakini wakapanda siku hadi siku hadi kufikia hatua ya kufanya biashara kubwa.

Related image

Everlne Rukanda, Baada ya kumaliza chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliamua kujiajiri na kujiingiza kwenye ujasiriamali wa biashara ya kutengeneza samani akifungua kampuni yake ya Evelyne Furniture.

Anasema aliipenda kazi hiyo kwa vile ilikuwa inakwenda sambamba na kazi yake ya awali ya  kutengeneza mito na maua na kutoa ushauri wa mpangilio wa nyumba kwa malipo..

Anasema ilifika wakati ambapo aliamua kutengeneza kabisa sofa kwa ajili ya kuwauzia wateja wake ambao waliipenda sana huduma hiyo. “Nilipoona nazidi kupata kazi nyingi nikaamua kuondoka nyumbani kwa wazazi kule Ubungo na kwa hiyo nikaamua kufungua ofisi Namanga hapo nilikuwa nauza mito na maua na kutoa ushauri wa upambaji wa nyumba kabla ya kuanza kutengeneza masofa,” anasema.

Image result for furniture sofa

 

Aliamua kuhamisha biashara zake eneo la Namanga na kuhamia katika eneo kubwa lililopo karibu na Mikocheni Macho ambapo kwa sasa ameweka bidhaa zake anazotengeneza zote kwa pamoja kuanzia, mito, maua na fenicha ili kumvutia mteja kuona kazi zake kwanza.

Image result for MAUA YA UREMBO

Kuhusu bei, Evelyne anasema alikuwa akitengeneza mito mikubwa na midogo na kisha kuiuza kwa Sh 15,000 hadi Sh 25,000 na kwamba mbinu aliyoitumia ilikuwa ni kuiweka katika mitandao ya jamii mito aliyoitengeneza kwa mara ya kwanza na alifanikiwa kwani alianza kupigiwa simu na wateja tangu siku ya kwanza ya biashara hiyo.

Anawashauri wanawake kutochagua kazi na hasa wahitimu wa elimu ya ngazi yoyote kuanzia ya sekondari, vyuo na hata vyuo vikuu huku akiwataka kujenga zaidi hali ya kujiamini katika kujiajiri.

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com