Njia za asili za kukabiliana na kwikwi.

Kwanza inabidi tujue kwamba Kwikwi ni tendo lisilo la hiari la kusinyaa kwa kiwambo cha mapafu (diaphragm) likifuatiwa na kufunga kwa haraka kwa koromeo linalopitisha hewa.

Nini husababisha Kwikwi

Kuna sababu kuu mbili zinazopelekea mtu kupatwa na kwikwi ambazo ni kula na kunywa kwa kupitiliza. Ulaji wa chakula au unywaji wa vimiminika kwa kiasi kikubwa husababisha tumbo kutanuka kuelekea chini na kujikandamiza dhidi ya kiwambo (diaphragm) ambako hupelekea kuanzishwa kwa mtetemo wa kwikwi.

Sababu nyingine zinazpolekea wewe kupatwa na kwikwi ni Kula chakula kwa kasi kubwa,Kuhamaki kwa hasira pasipo na sababu kubwa, Kula chakula kusikofuata ratiba maalum.

Kunywa vinywaji vya chupa kama vile soda, Msongo wa mawazo au mshawasha juu ya jambo fulani, Kuoga maji ya baridi sana, Kuvuta sigara, Kunywa pombe kali.

Njia za asili za kukabiliana na Ugonjwa wa kwikwi

Njia zifuatazo zitakusaidia kukabiliana na kwikwi. Njia hizi zinahusisha kuifanya kwikwi kutulia kwa kufanikiwa kupindisha njia ambayo inapelekea kwikwi kutokea.

Chukua bahasha kubwa (A6). Hizi zinapatikana maduka ya vifaa vya ofisini, rangi ya khaki. Uweke mdomo wako katika bahasha, hakikisha unaziba vizuri pasiwe na namna hewa inaweza kuingia ndani ya bahasha. Pumua ndani ya bahasha, kwa kuvuta na kutoa hewa mara 10, mpaka uhisi kuishiwa pumzi. Unapopumua ndani ya bahasha, unatengeneza hewa ya ukaa ambayo hufanya kikwazo cha kwikwi.

Related image

Vuta hewa na ishikilie katika mapafu kwa kadiri unavyoweza kisha imeze unapohisi kwikwi inataka kurejea tena. Fanya hivi mara 2 mpaka 3. Baada ya hapo tulia na rudia tena.

Vuta na shikilia hewa katika mapafu yako kwa muda mrefu kadiri unavyoweza kisha iachie kwa kupumua taratibu.

Pumua taratibu, ukiwa umekaa wima kadiri uwezavyo,

Ishikilie hewa katika mapafu yako huku ukiinamisha kichwa kwa nyuma mpaka umbali unaoweza.

Jaza maji ya kunywa katika glasi, inama kuelekea mbele kisha kunywa maji hayo kinyume.

Simama nyuma ya mtu mwenye kwikwi, akiwa ameketi katika kiti. Ishike shingo yake taratibu kwa kutumia vidole vyako kisha mkande kande upande wa nyuma wa shingo yake, kila upande wa uti wa mgongo, kwa kutumia vidole gumba.

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com