Niliandika Kitabu nikiwa na umri wa miaka 7-Serita Turner.

Anaitwa , Serita Turner mzaliwa wa Kenya ambaye ni mmoja wa wasichana wadogo wenye kipaji kikubwa cha uandishi wa vitabu.

Kitabu chake cha kwanza aliandika akiwa na umri wa miaka saba.

Kwa sasa ana umri wa miaka 11, alikipa kitabu hicho jina la ‘Adventures Bring Change’.Kitabu ambacho aliwalenga watoto wenzake na kilikuwa na maudhui ya kujenga umoja na mahusiano mazuri ili kubadilisha jamii yake.

Alipenda kuona watu wote wakishirikiana pamoja na kuondokana na tatizo la ukabila na ubinafsi ambao ulishashaota mizizi na kusababisha matabaka makubwa.

Aliona kuwa watoto wanaokwenda shuleni  kila siku ndio msingi mkubwa wa kukabiliana na hali hiyo.

“Ili kukuza ushirikiano wa kitaifa na umoja nchini, tunapaswa kuanza na watoto wa shule ili kuwafundisha wema na uzalendo wa kitaifa”

Anasema kuwa ingawa kitabu kiliwalenga watoto zaidi, lakini pia kinaweza kuwafaa na watu wazima ambao wanahimiza ubinafsi na ukabila.

Anasema kuwa alivutiwa na aliekuwa rais wa Marekani, Barack Obama ambaye ana asili ya Kenya.

Pamoja na kuwa raisi katika taifa kubwa la Marekani hakuwatenga wakenya na kutoa misaada mingi nchini humo bila kuangalia tofauti za makabila au rangi.

Kutokana na jitihada za Serita kwa sasa ni mmoja wa mabalozi wadogo wa masuala ya amani na umoja  nchini Kenya na Afrika  kwa ujumla aliependa kila mtu ajione yuko sawa na mwezake.

Tunahitaji wakina Serita wengi zaidi ilikuwa  na Afrika nzuri zaidi.

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com