vitu 5 nilivyo jifunza kwa kuuza bidhaa moja tu iliyoendesha maisha yangu yote kwa mwaka mzima

 

Ukiweza kupata biashara moja itayo kulipia kodi ya nyumba, kukulisha, kusomesha ndugu zako wawili watatu, kukutoa out kila weekend, kukuvalisha, kulipa madeni yako yote basically kwa biashara moja, sio hata biashara moja, bidhaa moja tu, ukawa hauna hofu yoyote ya maisha kwa mwaka mzima utajiskiaje?

Well mi nimesha experience hii ilikua kama mwaka 2014 flani hivi wakati ndio kwanza naanza kujifunza kufanya biashara na hii ndio ilikua bidhaa ya kwanza kufanikiwa.

Nakumbuka siku za mwanzoni kabisa ambayo niliagiza piece 20 tu ya bidhaa hii, na kuuza zote ndani ya siku moja tu, simu nilipigiwa na watu zaidi ya hamsini wanaotaka hii bidhaa, nilichoka kupokea simu mwenyewe. Watu wana furahi kweli kwa kuwa walikua wanatafuta hii bidhaa miaka nenda miaka rudi, watu wengine wakataka kuongeza hadi hela ili wapelekewe mda huohuo, wengine wanasema “uko wapi nakuja sasahivi”. Nikiwa kama mtu ambae naanza tu kwa kipindi hiki, siijui biashara vizuri na naskia kila siku watu wanavyofeli, hii ilikua kitu cha kushangaza sana.

Hamna mwaka niliyokua busy kama mwaka huu, niliuza mkoa niliokuepo (dar), nikasafirisha mikoa mingine (karibia mkoa yote nimetuma, mikoa mingine hata majina yake nilikua sijaishika kichwani). Nikaanza kutuma hadi nchi za jirani, nikaanza kuuzia maduka kwa wholesale, na nikawapa madogo flani waliokua mtaani kazi ya kuwapelekea watu popote walipo kwa mwaka mzima na commission yao ilikua nzuri tu, kwa kweli huu mwaka ulikua mzuri sana kwangu uki linganisha na miaka mingine iliyopita kabla ya hapo.

Anyway bila kupoteza mda bidhaa ni hii hapa.. watu wanapenda ku iga wakishajua kituflani kimefanya kazi kwa mwingine lakini there is alot that goes into “kuuza a product haraka, kama hivi” so good luck.

 

Image result for armband

Ngoja kidogo. Here is the story of how nilipata hii Bidhaa.

Kama percent kubwa ya watu niliamka siku na kugundua kuwa inabidi nipunguze kilo kadhaa, ilikua asubuhi kweli nikaamua kutoka siku hiyo ili kwenda kukimbia, kitu kingine kuhusu mimi ni kwamba napenda mziki mno, mda wowote ukiniona kama siongei na mtu nina earphone maskioni naskiliza mziki, so it made sense kuwa nnapokimbia nitahitaji mziki, nikatoka na simu yangu na earphones.

Kama mtu ameshawahi kujaribu kufanya hivi atajua kwanini ilikua ngumu sana kukimbia huku umeshika simu, au hata kuiweka mfukoni, earphone na zenyewe zinajipinda kila saa yaani hadi inakera kutumia simu wakati unakimbia, so nikaendelea kama wiki hivi najikaza hivihivi , wiki inayofuata nikasema haiwezekani lazima kutakua na solution ya jinsi ya kusolve hii kitu nikaingia online na kuanza research dakika kadhaa zinazofuata nikakutana na mkombozi wangu wa mwaka huo.

But yeah, simu inakaa mkononi!!!!! this was a break through, nikaagiza piece yangu moja, kama wiki mbili zinazofuata nikaipokea. Next day nikaivaa na kwenda kukimbia, it was the best run i had in my life.

Nilivyorudi nyumbani akili yangu ya ki enterprenuer ikaanza kucheza…. what if? what if?.. Nikaagiza piece 20 hapohapo, sikuwa hata na hela ya kutosha ya kula the next day ila nikajitosa tu, it wasnt hela nyingi ila kipindi hiko money was tight, well kama wanavyosema “the rest was history”.

Kwa sahivi nimeona watu wengi sana wameingia na kuanza kuuza the same product, lakini i was the first. ukiona mtu anakimbia na amevaa armband mkononi, ujue kuna possibility kubwa kwamba imetoka kwangu.

Nikajifunza mambo mengi sana kwenye kipindi hiki na baadhi ni ya fuatayo

Image result for armband

 

Mambo 5 niliyojifunza kwa kufanya hii biashara.

1) Bidhaa ambayo itauza vizuri ni ile inayo rahisisha maisha ya watu
2) Hauhitaji duka kuwbwa kuanza biashara na kufanikiwa (ni bidhaa tu inayohitajika)
3) Wateja wapo wengi sana mtandaoni, bidhaa na wauzaji wachache.
4)Umuhimu wa kuwa na website na kuji brand vizuri
5) Competition really doesnt matter sana as long as kuna market

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com