Jifunze: Nilitumia mtaji wa laki moja kuagiza bidhaa kutoka China mpaka kufikia milioni 3.

Kuanzia mwezi wa 12 mwaka 2014 nilianza ku experiment na kuagiza vitu kutoka china, nimekutana na malalamiko mengi ya watu kwenye research yangu kabla sijaanza, watu wanalalamika kuwa wanaibiwa mizigo yao haifiki, au wakiagiza mizigo inayofika inakua siyo yenyewe na yenye quality ndogo sana.

Nikasema ngoja nijaribu na mimi nione expirience yangu itakuaje, nikaweka pembeni laki moja kwa ajili ya kuagiza vitu tofauti, nilikua sijui chochote kuhusu ku import, nini kinahitajika wapi pa kuchukulia mizigo, unasubiri kwa mda gani hadi mzigo uupate, maswali yalikuepo kibao kabla ya kuanza. Ila nikajitosa tu na mtaji wangu huohuo mdogo.

Kwa kutumia laki moja, niliagiza kama vitu 15 hivi tofautitofauti vya bei ndogo, kati ya hivi 15, 13 vilifika.. 7 kati ya hivi 13 ndo vikawa kama nilivyotarajia na vyenye quality nzuri, kati ya hivyo 7 vitu vinne tu ndo nikaona vitaweza kuuzika, kati ya hivyo vinne viwili tu vikauzika.

Image result for china products

Hivyo viwili, vikauzika na kuagiza vitano, vitano nikaagiza kumi, na kufikia sahivi naagiza mzigo wa hadi milioni 3 wa hiyo bidhaa kwa faida yake yenyewe ambayo sijaongezea hela za pembeni hata maramoja. Baada ya hiyo bidhaa moja kufanikiwa nikawa nimejifunza mambo mengi sana kuhusu kuagiza bidhaa na kuziuza kutoka nyumbani kwa kutumia mtandao tu.

Nika rudia hili zoezi kwa kutumia faida ya bidhaa ya kwanza, nikaagiza bidhaa mbili zingine, this time nikawekeza kama laki tano hivi kwa kila bidhaa, kati ya hizo mbili moja ikafeli, mabaki yake bado yame jificha kwenye kona moja nyumbani kwangu, bidhaa ya pili kati ya hizi ikafanikiwa na yenyewe, nikajifunza mengi zaidi kupitia hilo zoezi pia.

Nilijifunza jinsi ya kutengeneza demand ya bidhaa na kumaliza mzigo haraka zaidi, jinsi ya kujua bidhaa gani inahitajika kabla hata ya kuagiza, so sikuishia hapa nikajaribu bidhaa nyingine tena, kwa kutumia mambo yote niliyojifunza, this time i was right, mzigo wa piece mia ukaondoka ndani ya siku 3.

kwa kutumia njia zote nilizojifunza nikafanikiwa kuanzisha biashara mbalimbali za mtandaoni, bidhaa mbalimbali tofauti na kuweza kuziendesha kwa muda wa mwaka na zaidi bila hasara yoyote, bidhaa zote ninazo agiza zinapata wateja kwa wakati muafaka, nikafikia kipindi nikaanza kuwa nauza hadi nchi za jirani kwenda Kenya na Uganda.

Nikajifunza mengi pia kuhusu kusafirisha bidhaa nje ya nchi na kupokea malipo na mengine mengi. Sitoweza waonyesha biashara zangu zote  , lakini ntajaribu kuwaonyesha moja wapo tu ya biashara ninazoendesha.

Tuchukue mfano hapa chini

hii smartwatch inayouzwa na mtu kutoka jumia kwenye picha ya juu kwa tzs 120,000/= , ambayo ni the same smartwatch utayoweza kununua kutoka alibaba (cheki picha ya chini yake), site inayouza bidhaa kutoka china kwa bei nafuu ya 13.5$ ambayo ni sawa na karibia 30,000… at best case scenario huyu mtu ananunua kwa 30,000 na kuuza kwa 120,000 ambayo ni faida ya 90,000 kwa saa moja.. worst case analipia kodi mzigo ambayo takribani atakua ananunua kwa 50,000 ambayo faida itakua 70,000.

capture

So kwa product kama hii inayopata faida ya 70,000, au tusiende kote huko, tuseme umeingia kwenye soko la kuuza smartwatch hizi na ukauza kwa bei ya elfu 80,000 ambapo wewe utapata faida ya 40,000 tuseme, unahitaji wateja 25 tu kwa mwezi kuweza fikisha faida ya milioni moja. Na uzuri wake hauto hitaji kuanza hata na smartwatch zote 25, unaweza ukaanza na moja tu, ikauzika then ukanunua mbili zikauzika, then tano, then 10, then 25. Ukifika 25 unaweza baki hapo maana umefikia target yako, na kuendelea kula faida ya milioni moja kila mwezi.

So kwa kifupi bila kupoteza muda zifuatazo ndo step 10 unazoweza kuzifuata ili kufikia

  1. Tafuta product ambayo itahitajika na watu kadhaa- huhitaji hata wateja wengi, kama product ina faida ya 20,000.. ukiwauzia watu 50 tu kwa mwezi una milioni moja.
  2. Testing phase, jaribu soko kama bidhaa utayoileta itahitajika na wateja
  3. Agiza kutoka china au nchi ambayo vitu vipo kwa bei rahisi (bila kupotea wala kuibiwa).
  4. Tafuta brand / jina la bishara yako (tengeneza logo/header photo n.k)
  5.  Tengeneza outlet zako (social media accounts, facebook, twitter, instagram, website (siyo lazima lakini ni muhimu) pamoja na number ya simu na whatsapp itayokuwa hewani mda wote.
  6.  Tafuta outlet zingine za kusambaza product (jumia, kupatana,olx n.k) pamoja na groups za facebook.
  7.  Jua msimu wa bidhaa zako/ jua mda na siku gani ambayo ni nzuri kutangaza bidhaa zako.
  8. Tangaza kwa bei rahisi kama utahitaji kufikia wateja wengi zaidi na haraka zaidi ( kwa kutumia matangazo ya facebook/instagram/google ads).
  9. wapatie wateja bidhaa zao.
  10. Save contact za wateja ukipata bidhaa mpya unawatumia kwa whatsapp/message

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com