Ushuhuda: Nafurai ila najutia sana.

Bored Young Woman Stirring Coffee --- Image by © Vincent Mo/zefa/Corbis

Ukweli ni kwamba niliachwa na mume wangu kwa kosa ambalo hadi leo hii sijaelewa kwanini lilinivunjia ndoa.

Nilimpenda sana mume wangu nilimuheshimu sana ila cha ajabu sikuridhika kuwa naye. Nakumbuka kabla hatuja funga ndoa tulipendana hadi watu wakashangazwa na upendo uliokuwa kati yetu,ila baada ya kufunga ndoa tu hatukuwa na amani.

Image result for lonely black women

kila siku ya Mungu kulizuka jambo jipya lakini mume wangu hakujali vituko vilivyokuwa vinatokea katika ndoa yetu isipokuwa hili lililofanya tuachane.

Najua wataka kujua ni jambo gani lilifanya tuachane, jambo hilo ni kutoridhishwa na mume wangu.Ni ajabu ila ni kweli sikuridhika naye.

Nililelewa katika familia tajiri sana sikuwahi kufanya kazi hata kuosha viombo,nilikuwa nafuliwa mpaka nguo za ndani ila nilivyokutana na mwanaume huyu chuoni macho yangu hayakutazama umasikini wake bali upendo wake.

Image result for lonely black women

Mwanaume huyu niliyempenda siye mume niliye achana naye bali ni mwanaume niliyenaye baada ya kutambua kuwa niliyefunga ndoa naye japokuwa nampenda na kumuheshimu hakuweza nitimizia haja yangu ya moyoni ambayo ni upendo wa dhati.

Kwasasa nipo na ninayempenda kwa dhati ,ingawa si tajiri kama alivyokuwa mume wangu ila ni tajiri wa moyo wangu.

Unajua ilikuwaje sikutaka kufunga naye ndoa na kukimbilia kwa mwanaume huyu nileye achana naye?

Ilikuwa ni ushauri ushauri wa mashoga zangu na sio watu wengine na wala sio wazazi wangu ila ni marafiki zangu.

Nakubali nilikuwa na wanaume wawili enzi zile, ila nilikuwa njia panda pale wote walipotaka kunioa ndipo rafiki zangu wakanishawishi kuwa na mtu mwenye mbele(future) kuliko kutaabika.

Ndipo nikatupia mbali ombi la yule nimpendaye na kwenda kwa huyu nisiyempenda kwa dhati.Najutia sana kwani ingependeza hata hawa watoto wawili nilio zaa naye ningezaa na huyu nimpendaye.

Nafuraha ila najutia sana.”

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com