Mtaji wa uenyeji, msingi wa biashara iliyobadilisha maisha yangu.

Watu wengi saivi hulalamikia  ukosefu wa ajira, mitaji lakini unatambua kuwa unaweza ukawa mwenyeji tu!  ikawa ni mtaji utakaoweza kukujengea chanell na kipato kikubwa na ukasahau kabisa kuajiriwa kama nilivyofanya mimi.

Mwaka 2012, nikiwa zangu home baada ya matokeo ya form 4, kutoka nikakutana na mzungu mmoja huyo bwana alikuwa ametokea Amsterdam ila katika maongezi nikashangaa akinambia kuwa hana nyumba wala sehemu ya kulala.

Image result for tourist in zanzibar

Basi nikajitolea nikampokea home nikawa nalala nae asubuhi tunaenda kutembea nikimuonesha maeneo mbali mbali ya jiji, katika maongezi yangu nikawa na lalamika sana kuhusu ajira huku nikiilalamikia malalamiko serikali.

Ndipo jamaa aliponielekeza fursa ambayo mpaka leo hii imenisaidia mengi na imenifanya nifahamiane na watu wengi sana duniani ishu yenyewe ni kupokea wageni mbali mbali kutoka nchi tofauti duniani (watalii).

 

Image result for tourist in tanzania

Kwani wengi huwa hawajawahi kufika Tanzania au Kenya hivyo hutafuta mwenyeji wao kwa ajili ya kuwatembeza sehemu mbali mbali pamoja na kuwapeleka kwenye vivutio mbali mbali kupitia site yao.

Basi akanielekeza nikajiunga na site hiyo, haikuwa ngumu kujiunga na ilikuwa ni rahisi sana. Basi nika search watalii ambao wanahitaji watu ambao ni wenyeji kwa ajili ya kuwatembeza kwa siku wakaazo kwa Dar.

Kwa mara ya kwanza niliwapata 3, ambao walifikia gest ikawa asubuhi nawafata nawazungusha maeneo mbali mbali kama Zanzibar, Kilimanjaro, Tanga, Bagamoyo na Dodoma kwa Tanzania gharama za safari pamoja na chakula walikuwa wanazilipa wao kama wao na siku wakiondoka nilikuwa wananiachia  visenti kidogo mpaka dola 1500.

Wale ambao nilikuwa nikiwapokea wakawa wanaenda kuelezea na wenzao na kunifanya nizidi kufahamiana na wengine zaidi, basi hali ikaendelea kuwa hivyo kiasi cha kupata wageni mpaka 15 kwa mwezi, wengine walikuwa wana hadhi mbali mbali kama wanafunzi, madaktari nk.

Image result for tourist in tanzania

Kutokana na wingi wa watalii ambao nilikuwa nikiwapokea na kuzunguka nao maeneo mbali mbali nikajikuta nikiwa na marafiki wengi sana katika nchi mbali mbali duniani, urafiki ambao naweza kusema umeyabadili maisha yangu kwa sasa kwani nimepata mialiko sehemu tofauti duniani na misaada mbali mbali kutoka kwa watu hao ambao nilikuwa nikiwapokea.

Ndugu zangu tusitegemee tu kuajiriwa na serikali bali mtambue kuwa kuna fursa nyingne nyingi sana za kufanya na kufanikiwa cha muhimu tu inakupasa ujichanganye na watu na kuzitafuta
Namshkuru Mungu kupitia kazi hiyo nimeanza kujenga naendesha gari yangu mwenyewe na nimeweza kutembelea maeneo mbali mbali ndani na nje ya Tanzania, nimejijengea marafiki kutoka zaidi ya nchi 50 duniani, kiasi cha kusema nikitaka kwenda kati ya nchi 10 basi 8 ntakuwa na wenyeji au 10 zote ntakuwa na wenyeji.

Tunasubiria ajira ambazo hatujui tutazipata lini na tukiwa na umri gani hivyo wakati unasubiria ajira saka fursa nyingine
.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com