Nina Degree lakini natumia kipaji cha uchoraji kuendesha maisha.

Kila mtu anapopewa picha yake uso hujaa tabasamu jambo linalonifanya nijivunie kwa sababu sikufundishwa kuchora na mtu yeyote ila nilipokuwa mtoto nilikuwa nachora kujifurahisha.

Related image

Sikuwahi kuwaza kama siku moja itakuwa chanzo cha mapato yangu na nitaifanya kama ajira yangu rasmi na kuwekeza muda wangu wote kuifanya,’’

Kijana huyu, Christian Chrispin, alihitimu Chuo cha U simamizi wa Fedha (IFM) Dar es Salaam na kuamua kuweka vyeti vyake kwenye kabati ili kutumia kipaji chake cha uchoraji na kuweza kupata mafanikio.

Aliona hakuna haja ya kuangaika kutafuta ajira kama ambavyo vijana wengi baada ya kumaliza vyuo wakiangaika, alijiona ni mtu anayeweza kupata mafanikio kupitia kipaji chake cha kuchora na kuamua kujitolea maisha ya uchoraji.

Image result for pencil picture of nyerer

 

Alianza bila mtaji wowote kwa kuchora picha za watu maarufu kama wanasiasa wasanii na kutumia mitandao ya kijamii kama Instergram,watu walivutiwa nazo na kuzinunua.

Baada ya hapo alianza kupata wateja waliohitaji na wao kuchorewa na hapo ndipo biashara ilianza kukua na kupata wateja wengi waliohitaji kuchorwa.

Anasema picha moja huweza kuchora kwa Tsh 80,000 na inaweza kuchukua siku tano kukamilika lakini bei hiyo inaweza kuongezeka inategemea na ugumu wake na rangi ambazo mteja anataka ziwekwe.

Anasema utafauti wa picha zake na wachoraji wengine ni kuchora picha za sura za watu kwa uhalisi na kuzifanya zionekane hai, na ili kuweza kufanikisha hilo aliamua kutumia muda wake wote katika uchoraji ili kuweza kumfurahisha mteja wake.

Image result for pencil picture of nyerer

 

Anaamini uchoraji ni njia ya yeye kufanikiwa na kupata maendeleo aliyonayo ambayo ni pamoja ya kazi zake kufahamika ndani na nje ya nchi.

Ndoto zake za baadae ni kufungua shule kwa ajili ya kufundisha watoto wadogo kuchora ili kuweza kurithisha kipaji alicho nacho na kusaidia watoto wenye kipaji hicho kukuza vipaji vyao.

 

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com