Wataalamu wametaja hizi aina 5 za kuonesha mapenzi. Je mpenzi wako anapendelea ipi?


Wataalamu wa masuala ya mapenzi wamesema kuna lugha tano za mapenzi na ni vizuri ukajua ni ipi ambayo mpenzi wako anaipenda zaidi umpatie.

Maneno matamu (Words of affirmation)

Hii ni ile hali ya kumpa mpenzi wako maneno matamu matamu ya kimahaba.

Maneno haya yanaweza kuwa, kuelezea hisia zako, vile anavyokufanya ujisikie, na maneno mengine ya kumfanya ajisikie kupendwa na muhimu.

Mguso (Touch)

Pengine mpenzi wako anapendelea kushikwa mkono mnapotembea.

Kama mtu anapenda kuguswa guswa ndio ajue unampenda halafu wewe unamfanyia mengine… UTAACHWA😂

Zawadi (Gifts)

Je mpenzi wako ni yule anayependa vijizawadi zawadi?

Inabidi ujue kama hii ndio njia yake ya kuonesha upendo ili ucheze mulemule na uweke tabasamu lake mahali pazuri.

Ku-spend time pamoja (Quality time)

Je mpenzi wako anapenda uwe karibu mara nyingi? Je hiki ndio kitu kinaweka furaha yake juu?

Kuna baadhi ya watu hataki vitu vingi wala maneno mengi, yeye anataka tu ukae nae.

Huduma za vitendo (Sex na vingine)

Je mpenzi wako ni yule ambaye anaoneshwa upendo kwa huduma nzuri ya mikuno kitandani?

Pengine sio huduma hii pekee inayomfanya ajue unampenda, so jifunze kile kinachomfurahisha na ukifanye.

Kila mtu ana namna yake ya kuoneshwa upendo. Sasa wewe ni bora ujue kile ambacho kinamfurahisha wako ili ujiweke kwenye nafasi ya kufurahiwa pia. 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com