naokota chupa kama kichaa lakini napata faida.

Biashara ya kuokota chupa mitaani imekuwa ikichukuliwa ni biashara ‘kichaa’ inayofanywa na mateja (Watumiaji wa dawa za kulevya)  lakini sio kama ilivyo kwa kijana aliejitambulisha kwa jina moja tu Gamanieli.

Watupipo  ilikutana na kijana huyu mitaa ya Mwenge Jijini Dar es Salaam na kuhadithia namna biashara hiyo ilivyompa faida na changamoto mbalimbali alizokutana zao ikiwa ni pamoja na kunusurika kupigwa kwa kudhaniwa mwizi.

watupipo.kifupi tuambie Biashara hii ulianza lini na inakulipa vipi.

Gama. Nilianza biashara hii kitambo kidogo mwaka 2008 nikitokea Same Kilimanjaro na katika kupita pita kwangu nikitafuta kibarua si unajua hapa mjini bila kupata miambili mia tatu huishi nilikutana na kijana mmoja anaeoktota chupa za plastiki na kunishawishi kufanya biashara hiii baada ya kuelewa faida yake.

Sikuwahi kufikiria kufanya biashara hiii lakini nilijikuta nikivutiwa kutokana na upatikanaji wa fedha yake kiwa haraka.

Baada ya kushawishika kama masihara kesho yake nimebeba mfuko wangu na kuanza kukata mitaa kutafuta chupa hizo, na kwa siku hiyo ya kwanza ndani yamasaa manne niliweza kukusanya chupa za sh.4000.

Nikaendelea na siku hiyo nikajikuta naingiza sh,15,000 kimchezomchezo tu.Nilikuwa nauza kilo moja ya chupa kwa sh.300 lakini wakati mwingine huchanganya na chuma na kuopata zaidi ya hapo.

Kuanzia wakati huo Gama ameweza kuendesha maisha yake vizuri akiwa amepanga na kuwa na mke pamoja na mtoto mmoja,Ambapo pia aliwesza kupata mtaji mdogo wa kufungua biashara ya matunda ambayo inamwingizia kiasi cvha fedha kuendesha gfamilia yake.

Watupipo:Nini malengo yako juu ya biashara hii ambayo wakati mwingine ukusanyaji wa chupa hizo huwa maeneo ambayo ni hatarishi kwa afya.

Malengo yangu sio kuendelea kufanya biashara hii maisha yangu yote bado natafuta fedha amabzo nazitunza ziweze kufikia kuanzisha mtaji wa biashara ambayo kidogo inastaha kama wa sh Milioni 5 hivi unatosha.

Watupipo:Changamoto za biashara hii kubwa ni zipi.

Gama: Kawa kweli zipo nyingi sana lakini kubwa zaidi ni kukutana na kadhia mbalimbali kama kudhaniwa mwizi ilishanitokea hiyo maeneo ya sinza nnikanusurika kuchezea kichapo na hii ni kutokana na baadhi ya waokotaji chupa wengine kutokuwa waaminifu na kuiba mali za watu.

nyingine ni za kawaida tu kudharaulika lakini mimi nimekuja kutafuta maisha hivyuo zidhani kama mtu akinidharau wakati naendesha maisha yangu itanipunguzia kitu nawaangalia vijana wenzangu wanapendeza lakini hata mia hawana halafu wajilinganishe na mimi nachafuka napata hjela na namudu familia yangu.

 

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com