Graduates: Kuna cha kujifunza hapa, nilianza na laki 3 sasa nina mtaji wa laki 8 ndani ya miezi 10

Nilipomaliza chuo niliajiriwa..bahati nzuri taluma yangu ina soko kubwa,so sikuona haja ya kufanya shughuli nyingine na hata hivyo ninatumika sana kazini..sasa bi mkubwa aliniambia anafikiria kufungua duka pale nyumbani.

Nilipopiga hesabu za faida ya kwenye kiberiti,sabuni za kipande,pipi nk..ni tsh 50,100,ikienda sana ni 1000 nk. niliona ni biashara kichaa..kwa kuangalia faida za namna hiyo niliona kabisa hata kulipia frem itakuwa mtihani..nilipolinganisha na salary yangu,nikamwambia,mke wangu subiri kwanza..lengo langu lilikuwa nimkatishe tamaa ili aachane na wazo lile..maana niliona kama that was too low kwa level yangu!

Mwaka uliofuata nikapata nafasi ya kwenda shule kujiendeleza kielimu..nilipoondoka tu bibie akachonga na mwenye nyumba wakakubaliana..akamwita fundi akaja akagawa sehemu ya sebule,akaweka frem!

Kisha akaniambia ule mpango wake wa duka hakuufuta ila kwa kuwa mimi ndio nilikuwa namwekea kauzibe na sasa nimeondoka,basi akaanza utekelezaji..sikukubaliana sana naye ila nilimwacha aanze ili akikwama nimzodoe kwa kuwa alikataa ushauri wangu wa kisomi!!

Related image

Nakumbuka alianza na tsh laki 4..tena wakati anaanza kibanda chake kilikuwa ni kati ya vile vidogo kabisa..na kama mnavyojua,wateja wengi wananunua bidhaa kwenye maduka yanayoonekana yamejaa sana..kwa hiyo kwa siku alikuwa anauza kati 20,000 hadi 50,000..yeye alikuwa anafungasha kwenye waduka ya jumla ya pale karibu ambayo wamiliki wake walikuwa wananifahamu kutokana na kazi yangu..kwa hiyo walikuwa wanamwamini na kumpatia mzigo anakuja anauza kisha anarudisha hela..

Nilipoona anaendelea,nikaanza kuvutiwa,niliporudi nyumbani likizo nikachukua mkopo benki nikampa 2mil akaongeza kwenye mtaji..baada ya miezi 6 akaanza kuuza vitu kwa jumla na reja reja..hapa kulikuwa na changamoto..kwa kawaida kuuza vitu kwa jumla faida inapungua,so unategemea zaidi mzunguko wa biashara..ukiwa na mzunguko mzuri ndo faida inaonekana..

Mwanzo wa wazo la kuuza jumla lilikuwa kufanya biashara na wenye frem wenzetu wa hapa kwetu..lakini haikuwa hivyo..pamoja na kwamba tulikuwa na vitu vingi vya muhimu lakini hawakupenda kuja kufungasha kwetu..

Walikuwa tayari kwenda mjini tena bila kujali kwamba gharama ni kubwa kuliko kama wangefungashia kwetu..bibie alikuwa anaongea na wengine anawaambia wachukue mzigo wakauze na kurejesha hela kama alivyoanza yeye,lakini bahati mbaya walikuwa hawaonekani tena baada ya hapo!

Baada ya kuona kama tunauza sana,kuna watu watatu nao walifungua maduka ya jumla hapa hapa..wakawa wanauza bidhaa zama tunazouza..ushindani ukawa mkubwa mauzo yakashuka..tukaendelea kumwomba mungu..lakini haikupita miezi 6 biashara ikawashinda wengine wakafunga kabisa na wengine wanauza tu kwa reja reja..

Kiufupi,pamoja na kumfanyia mtima nyongo,gharama na maisha yangu ya shule yaliendeshwa na biashara ya bi mkubwa..kwa sasa mtaji wa duka lake ni zaidi ya 50mil..ana duka dogo la nguo,amejenga,kuna viwanja na mashamba kadhaa na mimi binafsi nina mishe zangu ninazoendesha;vyote hivyo si kwa sababu ya mshahara wangu,bali kutokana na bisashara za bi mkubwa..nasema hivi kwa sababu mshahara wangu hautoshi hata kulipia ada ya watoto,chakula na maisha ya familia ya kila siku.

Nilichojifunza ni kwamba,spirit ya ujasiriamali mtu anazaliwa nayo..huku ukubwani tunaiga tu na ndio maana wengi tunafeli..na hasa kwa hawa tunaojiita wasomi ndo kabisaa..maana tunapoanza tunataka tufanikiwe kesho;kitu ambacho hakiwezekani..vile vile wasomi hawapendi ku’take’ risk..mtu anafikiria zaidi hasara badala ya faida ndogo ya kuanzia..

Pili,ni uaminifu..watu wengi wanasema wafanya biashara wakubwa si waaminifu;kwa maana kwamba waliofanikiwa wamefanya hivyo kwa kudhulumu wengine..ila mimi nasema kama unaanza,hakuna namna utafanikiwa bila kuwa mwaminifu..ukishaaminiwa,huo ni mtaji namba moja..bi mkuwa ametoka kwa sababu walikuwa wanamwamini wanampa mzigo anakuja anauza na kurejesha pesa ya watu..ila kuna wale aliokuwa anawaamini,anawapa mzigo,wakiondoka hawarudi tena..mpaka leo wako palepale na wanatia aibu kweli..

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com