Mtoto wa kishua aliyeuza maji ya kandoro na kupata laki nane kwa siku tatu.

Kwa kifupi mimi ni kijana wa miaka 29 nimezaliwa kwenye maisha ya kishuani huko Arusha ila nilifukuzwaga nyumbani toka 2006.Hapo ndo nilipopata changamoto za kufanya biashara za mitaji midogo.

Katika biashara nilizowai kufanya zote nilifanikiwa.Niliuza nguo za kike chuoni,pipi maji ya kandoro na sigara nyakati maalumu,matofali ya kuchoma,dagaa wa kuosha,banda la chips,Laystation (kuchezesha magemu)

Nyingine nashindwa kuziorodhesha kutokana na kupitwa na wakati na sitoweza  kuchambua zote ila nitaanza kuchambua moja kwa sasa.

Biashara ya kufunga maji (Kandoroo enzi zile) na sigara kipindi cha sabasaba au nane nane siku 7 na 8 za mafanikio.

 

Image result for water in plastic

 

 

Nilipewa wazo toka kwa house boy aliyefukuzwa home kwetu  miaka mingi.Lilikua wazo gumu kwangu tokana na maisha niliyokulia ila nilijikaza nikafanya.

Nilianza na mtaji wa 70,000 ilikuwa Morogoro.Kwanza niliazima meza mbili kwa ajili ya kuwekea pipi,nilikodisha ice box mbili kwa ajili ya barafu,nilinunua ndo 8 za maji, nililipa kitambulisho cha mfanya biashara ili kupunguza gharama za kulipa kila nikiingia langoni mwa uwanja wa nane nane.

Image result for water in plastic bag

Nilinunua vifuko vya kufungia maji vya kutosha, nilinunua chujio kubwa na katika hii biashara ya maji ndo ilinipa pesa nyingi wakati huo ndoo moja ya maji ilikuwa ikiuzwa Sh 100.

Sikumbuki mahesabu yote kwa uhakika ila siku ya kwanza niliuza maji elfu 9 ikiwa kandoro moja ni tsh 50 wakati biashara ya pipi na sigara ikisua sua, siku ya pili niliuza maji ya elfu 12 biashara ilienda vizuri lakini ugumu maji yaliisha sikua na uwezo wa kufunga huku nikiuza biashara ya pipi jion yake nikamualika mshikaji (house boy) usiku tukafunga maji mengi sana.Siku ya tatu tuliuza elfu 24.

Jioni ya siku ya tatu.
Nilipata moyo sana nikaanza kuona faida ya biashara niliyokua naidharau.
Basi tukapata wazo la kuwaajiri vijana wanne kutoka kitaa usiku tunafunga maji asubuhI mpaka jion tunafanya biashara ya kuuza tu.Pamoja na kufunga maji mengi sana biashara ya pipi na sigara nayo ikachanganya sana.

Image result for biashara ya pipi

 

Hakika mpaka inafika tarehe 5 tulikua tunauza mpaka maji ya Sh 100,000 mwaka huo Mungu alijalia jua lilikua la maana.maajabu ni tarehe sita saa 6 mchana maji yote yameisha na watu wanataka tuwauzie hata kwa glasi. Hapo ndo tulipopiga pesa wadau. Zile cooler box zilikua na kitu kama kabomba. Tukazijaza maji na barafu tukanunua na vikombe 10.

Sisi kazi yetu ilikua ni kujaza barafu na maji tu.Kila glas ya maji sh 100. Uongo dhambi kama kuibiana lazima siku hiyo niliibiwa sana ila sikujali. Usiku wa tarehe nane tulilewa sana na vijana wangu.asubuhi ya tarehe 9. Ndio nikapiga mahesabu nimebaki na laki 8.

Nikagawa laki 2 nikabaki na sita. Pipi zilizobaki nikaziuza kwa bei ya jumla kwa muuza duka elfu 50 tukasambaratika tarehe 10.

Hivyo wadau kama kweli unania usivunjike moyo kufanya kitu kitakuzalishia faida tu.Pamoja na hayo pia kulikuwa na changamoto nyingi sana. Mfano sehemu ya kupanga meza zilikuwa zinapangishwa kwa zaidi ya mtu mmoja. Mwenye nguvu ndiye anafanya biashara.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com