Hatua 3 za kupata idea ya biashara ya kuanzisha anywhere.

Siwezi kukwambia hizi ndio mbinu za kupata idea ya kuanzisha biashara, lakini;

Hizi ni steps za mwanzo ukizitumia utaweza kujiongoza katika kusaka na kupata idea ya biashara.

Angalia vitu unavyopenda kwa sasa

Kuna vitu ambavyo wewe unapenda kuvifanya, au vitu ambavyo hutajali kujifunza kwa haraka. Kama kitu unakipenda ni rahisi kuanza hata kama hujakijua saana, utaendelea kujifunza as you do it.

Unapofanya kitu ambacho unakipenda na una hamasa ya kukifanya ni moja ya siri ya mafanikio, kwani utakomaa nacho hata ikitokea mambo hayajaenda vizuri.

Panga balance ya kazi na mapumziko

kazi yako utaifurahia zaidi kama utapata muda wa kupumzika, hivyo katika kuchagua idea angalia biashara ambayo itakua na balance ya maisha yako na kukuweka huru huku ikiendelea kufanikiwa.

Usitafute kujiajiri mwenyewe halafu ukajikuta umejiweka kitanzi na kufanya kazi masaa 24. “UTACHUKIA HIYO BIZNA NAKWAMBIA”

Utafiti

Hiki ni kipengele muhimu sana. Lazima ujue JE KUNA WATEJA? JE KUNA MTAJI WA KUTOSHA? JE KUNA GHARAMA ZA SERIKALI NA VIBALI? WILL YOU AFFORD?

Fanya utafiti na ujue kila kitu kuhusu biashara yako na vile utakavyo iendesha.

Utafiti unaweza kuufanya kwa kuuliza watu wanaofanya hiyo biashara, kufuatilia mwenyewe au kutafuta wataalamu wakusaidie kufanya utafiti fresh zaidi.

Endelea kuchakarika mkali maisha sio serious kihiiivyo.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com