Kinadada Haya ni Madhara ya Kuolewa na Mume Tajiri.

Mabinti walio wengi hutamani sana kupata wenzi wao wa maisha yaani waume wenye uwezo mkubwa kifedha, mume ambaye ana nyumba nzuri tayari, gari la kutembelea na mazagazaga mengine kibao yanayoonyesha maisha ya kifahari na starehe.
Lakini nyuma ya pazia kuna mambo wasiyoyajua yanayowapata wake wa matajiri ambao kwa nje wanaonekana wenye furaha wanaishi vizuri na wanafurahia maisha wala hawana shida yeyote.
Inaweza ikawa hivyo kwa nje lakini kihalisi kuna mambo ambayo walio wengi hawafahamu hutokea kwenye ndoa za matajiri na hivyo mabinti wengi kuwa na ndoto za kuishi kitajiri na kufanya bidii kupata mume wa ainahiyo na kisha kuvunjika moyo mara baada ya kukutana na hali halisi

je wajua kuwa,

1.wake wengi wa matajiri wana magari mengi ndani ya nyumba lakini huenda hajui hata ndani yake panafananaje zaidi ya kuyashika kwa nje tu au kuyaona tu yale pale yamepakiwa?

2.maneno ya kumsimanga mtu kama vile unajua gharama ya hivivitu wewe,?au ulivionea wapi hivi vitu wewe,unayajulia wapi haya mambo,vyakula hivi,kwenu uliviona ?na mengine mengi ni ya kugusa?

3.wake wengi wa matajiri hawana nafasi ya kuhoji mume anashinda wapi na nani, majibu yanayotolewa hapo, unafikiri haya maisha unayoishi hapa yanakuja tu hivihivi, unafikiri tukikaa kuangaliana sura utaviona vyote hivi?

4.wanaume wengi matajiri hawaishi masimango kama vile unishukuru mimi bila mimi usingekuwa hapo ulipo wala watu wasingekutambua,ulikuwa na nini cha maana,nimekutoa ukiwa huna mbele wala nyuma(hata kama kwa kweli alikukuta unajiweza kwa kiasi Fulani)

5.Wanaume wengi matajiri hawana nafasi ya kuonyesha upendo, kukaa na kuwajali wake zao, mara nyingi wako bize na shuhguli zao na hatamke akiomba walau apate nafasi ya kukaa na mume waongee mawili matatu, mume anajibu huli, huvai unalala chini? hayo ndo majibu.

6.Mara nyingi wake za matajiri hawashirikishwi kikamili au hata kidogo kwenye shughuli zinazowaingizia waume zao utajiri huowalionao, pengine hata kama mume ana kazi basi mke kamwe hawezi jua mapato ya mume wake kwa mwezi yakoje.
Jamani mabinti hayo ni machache tu yaliyo nyuma ya pazia kwenye nyumba za matajiri walio wengi.

Kwa hiyo tahadhari kwa mabinti usitamani sana kumpata mume tajiri kwa kujua kuwa ndo furaha ya maisha, japo sio vibaya kupata mume anayejiweza, tena ni vizuri zaidi kuolewa na mume mwenye uchungu wa maisha na malengo ya baadaye ya maisha yenu na watoto wenu.

Mbaya ni hii tamaa waliyonayo mabinti wengi ya kutaka kuolewa na mume tajiri sio ndoto nzuri sana, mengi yamejificha na kwa kuwa kuta haziongei ndo basi tena mume na mke matajiri wakitoka wameshikana mikono, tabasamu pana unadhani wameyamaliza maisha kumbeni ni siri ya kuta za nyumba zao.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com